Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Ni siku nyingine nzuri sana ya leo ambayo tumepata nafasi ya kipekee kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora.

img-20161217-wa0002
Msingi wetu mkuu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, kwa msingi huu tutaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu USIKUBALI HARAKA…
Moja ya vitu unahitaji kwenye haya maisha ni ubishi.
Kwa sababu hakuna chochote utakachokipata kwa urahisi, HAKUNA.
Kila utakachojaribu kwa mara ya kwanza utakwama au hutapata kile ulichotaka.
Sasa ukiwa mtu wa kukubali haraka, utakata tamaa mapema na hakuna kikubwa utakachoweza kufanya kwenye maisha yako.

Hata wale wanaokuletea taarifa mbalimbali, usikubali haraka, siyo wote wanaokupa taarifa kamili au taarifa sahihi. Wenginr huongeza au kupunguza mambo ili uchukue hatua wanazozitaka wao.
Ukiwa mtu wa kukubali haraka kila unachoambiwa na kila mtu, utajikuta unafanya maamuzi ya hovyo sana.

Chukua muda wako kuhoji na kuchunguza kwa makini.
Na kama umekosa kile ulichotaka, jua mbinu mbadala za kutumia kupata. Jua wapi unakosea na hatua zipi unaweza kuchukua.
Kukubali haraka ni kuamua dunia ifanye chochote kwako bila ya wewe kuamua au kuzuia, siyo njia bora.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.