Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.

img-20161217-wa0002
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo titafakari kuhusu NJIA BORA YA KULALAMIKA…
Mara nyingi yapo mambo ambayo yanatokea tofauti na tulivyotegemea. Au hayatokei kabisa wakati tulitegemea yatokee.
Unapokutana na hali kama hii, ni rahisi sana kulalamika, ni rahisi kukimbilia kusema nani angefanya nini ili mambo yawe vizuri.
Lakini hiyo siyo njia bora, kwa sababu unakuwa huna uhakika wa mabadiliko ya kweli.
Unaposema tu, haibebi uzito wowote na mambo yataendelea kama yalivyokuwa.

Njia bora kabisa ya kulalamika siyo kuongea, bali kufanya kitu, kuchukua hatua.
Kama kuna mambo yamekwenda tofauti na ulivyotegemew, basi chukua hatua. Fanya kitu kubadili hali hiyo ya mambo. Na kile utakachofanya kitachochea katika kuleta mabadiliko.

Unapoongea tu unaweka matumaini yako kwa wengine, ambao mara nyingi hawachukui hatua yoyote.
Lakini unapochukua hatua, una uhakika wa mambo kubadilika.
Hivyo mara zote, chukua hatua, fanya kitu.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.