Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

img-20161217-wa0002
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MAARIFA FEKI….
Moja ya vitu ambavyo huwa nawashauri watu kuacha mara moja, ni kuanza siku zao kwa kusikiliza, kusoma au kuangalia habari.
Siyo tu upotevu wa muda, bali pia ni kuvuruga utulivu wa akili yako. Unajikuta umejijaza hofu na huna tena hamasa ya kuweka juhudi kubwa.

Lakini watu hujitetea kwamba hawawezi kuacha kuanza siku yao kwa kufuatilia habari, kwa sababu kuna maarifa na mambo mengine muhimu wanayajua kupitia habari.
Wanaamini bila habari basi watakuwa wameachwa nyuma sana, watakuwa wamepitwa.
Hapa ndipo ninapowaambia ya kwamba, maarifa yoyote unayojishawishi unapata kupitia habari ni maarifa feki.
Kusoma au kusikiliza vichwa cha habari kwenye magazeti inakuongezea nini kwenye maisha yako?
Au kuperuzi mitandaonya kijamii na kuona vichwa vya habari au muhtasari wa habari kipinhasa unanufaika nacho?
Kuliko kupoteza muda wako mzuri kuhangaika na habari ambapo unapata MAARIFA FEKI, ni bora usome vitabu ambapo utapata MAARIFA HALISI.

Kadiri siku zinavyokwenda ndivyo wengi wamavyozama kwenye maarifa feki, epuka kabisa hilo na chagua maarifa halisi, yatakayokuwezesha kupiga hatua.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.