Katika jambo lolote unalofanya au utakalofanya, watu watakuwa na maoni yao juu yako na kile unachofanya. Maoni hayo yanaweza yasiwe yanayokupendeza wewe.

IMG-20170228-WA0007

Hata kama utakuwa unafanya jambo zuri kiasi gani, wapo watakaoona unafanya makosa, wapo watakaoona una kitu umeficha. Hata ukifanikiwa wapo watakaosema umetumia hila, wapo watakaosema umepata bahati.

Hivyo ninachotaka kukuambia rafiki ni kwamba, usisubiri kuongozwa na maoni ya watu, kwa sababu hata ukiacha unachofanya sasa na ukafanya kile ambacho watu wanasema, bado wapo watakaokuwa na maoni tofauti. Huenda wale ambao wa walikuwa na maoni yaliyokufanya ubadili, na wao wakabadili maoni yao.

Ufanye nini sasa?

Huna cha kufanya, kama lengo ni kuridhisha watu na wawe na maoni mazuri juu yako na unachofanya.

SOMA; Kila Mtu Ana Maoni.

Kama unachofanya ni sahihi, na ndiyo kinachokuletea matokeo bora, basi hicho ndiyo unaweza kufanya, endelea kufanya.

Endelea kufanya kilicho sahihi, endelea kuweka juhudi, na watu nao wataendelea kutoa maoni yao juu yako na unachofanya. Usijichanganye na kubadili chochote unachofanya ili tu uwaridhishe watu wawe na maoni mazuri juu yako.

Waongeaji huwa hawaachi kuongea, hivyo wewe mfanyaji endelea kufanya. Kila mtu aendelee na kile kilicho bora kwake, kwako wewe kilicho bora ni kufanya. Fanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK