Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Hongera sana kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu ambayo tunakwenda kuweka juhudi zaidi ili kuweza kupata matokeo bora.

img-20161217-wa0002
Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KWENDA KINYUME…
Mara nyingi watu husema kwamba hawana watu wanaoweza kujifunza kwao. Hawana watu wa kuwaongoza na kufika kule ambapo wamefika wao. Au waliofanikiwa, hawana muda au hawapo tayari kuwashirikisha mbiju zao.
Kwa kuwa jamii zetu zina watu wengi ambao hawajapiga hatua kubwa, tunabaki katikati ya kundi hili kubwa na kushindwa kufanya makubwa.

Lakini ipo njia inayoweza kukutoa kwenye kundi hilo na kukuwezesha kufanya makubwa sana.
Njia hiyo ni KUFANYA KINYUME na jinsi wanavyofanya wengine ambao hawajafanikiwa.
Unachopaswa kuangalia ni kipi ambacho wengi wanafanya, halafu azimia kutokukifanya.
Kama umeona wasiofanikiwa wanalala sana, wewe usilale kama wao.
Kama umeona wasiofanikiwa wana ndoto ndogo, wewe kuwa na ndoto kubwa.
Kama umeona wasiofanikiwa ni walevi, wewe usiwe mlevi.
Kama umeona wasiofanikiwa hawawezi akiba, wewe weka akiba.

Yaani kinyume kabisa, na baada ya muda utakuwa tofauti kabisa.
Kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, unajihakikishia kupata yale ambayo wao wanapata. Ili kupata matokeo tofauti, FANYA KINYUME na wengi wanavyofanya.

Kipi utaanza kufanya kinyume leo?

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.