Habari za leo rafiki yangu?

Karibu kwenye kipindi chetu kizuri cha ONGEA NA KOCHA ambapo tunapata nafasi nzuri ya kwenda kujifunza mambo muhimu kuhusu mafanikio kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla. Kama ambavyo nimekuwa nakuambia mara kwa mara, mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa, hakuna wa kukuzuia kufanikiwa, hala hakuna atakayekulazimisha kufanikiwa, ni hatua ya kuchukua wewe mwenyewe na kuyafikia mafanikio.


Katika somo letu la leo tunakwenda kujifunza Kanuni Moja Ya Uhakika Itakayokuwezesha Kupata Chochote Unachotaka Kwenye Maisha Yako.

Najua kuna kitu unakitaka sana kwenye maisha yako, na huenda siyo kimoja bali vingi. Huenda unataka sana fedha kwa sababu ya changamoto unazopitia. Huenda unataka kazi yako iwe na manufaa kwako. Huenda unataka biashara yako ikue zaidi. Huenda unataka mahusiano bora kabisa na wale wa muhimu kwako.

Ninachoweza kukuambia ni kwamba, unao uwezo wa kupata chochote unachotaka. Lakini kukuambia tu hivyo unaweza usiniamini, kwa sababu huenda umejaribu sana lakini hupati. Huenda hata umetumia njia zisizo halali, labda kuwadhulumu wengine au kudanganya, lakini bado hupati kwa uhakika.

Sasa leo kwenye kipindi unachokwenda kuangalia, nimekushirikisha kanuni moja ya uhakika ya kuweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako. Hii ni kanuni ambayo kwa kuweza kuitumia, utashangaa kila unachotaka kinakuja kwako.

Kanuni hii haiangalii elimu yako, umri wala rangi yako, ni kanuni inayoweza kutumiwa na mtu yeyote na anayeanzia popote. Angalia somo la leo kujifunza kanuni hii na kuweza kuifanyia kazi.

Kuangalia kipindi hichi kizuri cha leo bonyeza maandishi haya.

Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.

Nina imani utajifunza kitu muhimu sana, na utakifanyia kazi ili kuweza kuona matunda yake.

Kuangalia vipindi vingine vingi zaidi tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/video na kusikiliza vipindi vyangu vya sauti tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/podcast

Tuendelee kuwa pamoja ili tujifunze na kuboresha maisha yetu zaidi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.