Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo makubwa.

Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA, kasimamie hilo siku ya leo.
Karibu kwenye #TAFAKARI yetu ya asubuhi ya leo, ambapo tunapata kitu cha kwenda kuanza nacho siku yetu hii ya mafanikio.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUFANYA au KUTOKUFANYA.
Iko hivi rafiki, akili zetu huwa zinaturudisha sana nyuma kwenye mambo mengi. Na hii inatokana na tabia ya akili kupenda kutoroka.
Kwa mfano, unaweza kupanga kwamba muda fulani mpaka fulani utafsnya kitu fulani. Labda saa tatu mpaka saa nne utasoma kitabu. Muda ule unapofika na unaanza kusoma kitabu, au kufanya chochote umejipangia, akili yako haitulii, badala yake inaanza kufikiria vitu vingine ungeweza kufanya muda huo.
Na kama ulichopanga kufanya ni kigumu, basi akili yako itakuaminisha kuna kitu kizuri zaidi unaweza kuwanya.
Labda itakuambia angalia mitandao ya kijamii, kuna mambo yanakupita.
Au ongea na mtu fulani, hujaongea naye muda mrefu.
Akili itakushawishi hivyo, mpaka utaacha unachofanya na kufanya kingine, na ukishafanya hivyo tu, huwezi tena kurudi kwenye ratiba yako ya awali.
Tufanye nini kuondokana na hili?
Ili kuondokana na hili, na ili kuiendesha akili na siyo akili kutuendesha sisi, la kufanya ni moja tu. KUWA NA MSIMAMO.
Na msimamo huu ni hivi, JIAMBIE UTAFANYA KITU FULANI, AU HUTAFANYA CHOCHOTE.
Kwa mfano kama ulisema saa 3 mpaka saa 4 utasoma kitabu. Basi mids huo ukifika soma kitabu au usifanye chochote kile.
Yaani ni kushika kitabu na kusoma, na kama akili yako itaanza kukulaghai basi ni labda uendelee kusoma kitabu au uache na usifanye kitu kingine chochote kile.
Sijui umenielewa vizuri hapo rafiki🤔..
Yaani utafanya kile ulichopanga kufanya, au hutafanya kingine chochote. Utakaa pale mpaka uke muda uliopanga kufsnya kitu hicho uishe, bila ya kukimbilia kwenye mitandao au kufanya.
Kwa namna hii utaizuia akili yako kutoroka,
Na zaidi utaacha kuifuata akili yako kwa kila jambo dogo.
Muhimu zaidi utalazimika kufanya, kwa sababu utaona ni ujinga kukaa pale bila kufanya chochote.
Njia hii itaongeza sana ufanizi na uzalishaji wako, itumie kila wakati.
Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Leo ni KUTHUBUTU, USHINDI na SHUKRANI.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,