Habari za asubuhi ya leo rafiki?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.
Tutumie nafasi hii vizuri rafiki.

Asubuhi ya leo tunakwenda kutafakari kuhusu maneno sita muhimu yanayotuongoza kwenye maisha yetu ya mafanikio.
Maneno haya sita yamegawanyika kwenye makundi mawili.
Kundi la kwanza ni maneno matatu ambayo ni msingi wetu wa maisha ya mafanikio.
Maneno hayo ni;
1. NIDHAMU
2. UADILIFU
3. KUJITUMA.
Bila nidhamu hakuna kikubwa unachoweza kufanya.
Bila uadilifu hakuna atakayeweza kukuamini.
Na bila kujituma, huwezi kupiga hatua.

Kundi la pili ni maneno matatu ambayo yanatuongoza kwa mwaka huu 2017.
Maneno hayo ni;
1. KUTHUBUTU.
2. USHINDI.
3. SHUKRANI.
Uthubutu ndiyo utakaokuwezesha wewe kuchukua hatua ya kufanya makubwa.
Ushindi ni alama ya kuchukua hatua, ni kielelezo cha mafanikio.
3. Shukrani ni kukubali mafanikio yako, na kukaribisha mengine zaidi.

Andika maneno haya sita leo, na yaandike kila siku.
Kwa kuandika maneno haya, unayamiliki na inakuwa rahisi kwako kuyaweka kwenye vitendo.
Maneno haya sita hi muhimu sana kwa mafanikio yetu.
Tuyaandike kila siku, tuyaelewe na kuyaweka kwenye maisha yetu ya kila siku.

Uwe na siku njema ya leo.
Rafiki yako,
Kocha Makirita Amani,
MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA,
http://www.makirita.info