Ni imani yangu kwamba unaendelea vizuri na unaweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kwenye maisha yako.
Kama unavyojua rafiki, maarifa sahihi ni msingi muhimu sana wa mafanikio yako. Kwa sababu wapo wengi ambao wamekuwa wanajaribu mambo mengi, lakini kwa ukosefu wa maarifa sahihi hawafiki mbali. Au wanakutana na changamoto ambazo zinawarudisha nyuma kila wakati.
Ndiyo maana jukumu kubwa nililojipa mimi ni kukushirikisha wewe maarifa yote muhimu unayopaswa kuwa nayo, ili uweze kufanya maamuzi sahihi yatakayokufikisha kwenye mafanikio yako.
Ni katika jukumu hili nimekuandalia semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, elimu ambayo hatukuipata shuleni wala hatukuipata nyumbani. Elimu ambayo wengi tunaikosa na ndiyo maana licha ya kufanya kazi miaka mingi, bado tunakuwa na madeni na hatuna akiba za kutosha. Umefika wakati sasa wa kuondokana na changamoto hizo za kifedha, kwa kuwa na msingi sahihi wa fedha ili kuweza kujijengea utajiri.
Semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA itafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap, kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaanza tarehe 03/07/2017.
Lakini mwisho wa kujiunga ili kupata fursa ya kushiriki semina hii ni tarehe 30/06/2017. HIVYO RAFIKI, ZIMEBAKI SIKU MBILI TU, SIKU MBILI PEKEE. Nakusihi sana rafiki yangu, kama bado hujachukua hatua ya kujiunga, basi chukua hatua sasa, maana sitaki kabisa wewe rafiki yangu ukose semina hii muhimu na ya kipekee.
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada ya mwaka tsh 50,000/= kwa namba zifuatazo; MPESA 0755 953 887, na tigo pesa 0717 396 253, airtel money tuma kwenda tigo pesa 0717 396 253. Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253. Kumbuka unapolipa ada hii unapata maarifa kwa mwaka mzima, yaani ukilipa mwezi huu wa sita mwaka 2017 ni mpaka mwezi wa sita mwaka 2018.
Kama hukuwa umepata taarifa za kutosha kuhusu semina hii, basi hizo hapo chini ndiyo mada zitakazofundishwa kwenye semina hii;
SEMINA; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION)
FEDHA; DHANA HALISI YA FEDHA, UTAJIRI NA UHURU WA KIFEDHA.
Maana halisi ya fedha, utajiri na uhuru wa kifedha.
Mahusiano ya fedha na imani.
Jinsi unavyojizuia kupata fedha zaidi.
Kwa nini elimu ya darasani ni kikwazo kwenye fedha.
Namna ya kutengeneza fursa zaidi za kifedha kwenye maisha yako.
Sheria tano za fedha unazopaswa kuzijua na kuzisimamia.
KIPATO; NJIA ZA KUTENGENEZA KIPATO NA KUKIONGEZA.
Msingi muhimu wa kutengeneza kipato.
Umuhimu wa mifereji mingi ya kipato.
Mifereji ya kipato unayopaswa kuitumia.
Jinsi ya kukigawa kipato chako kwenye mafungu matano muhimu kwako.
Jinsi ya kudhibiti kipato kikubwa kinachoingia kwa mara moja.
Jinsi ya kuongeza kipato ukiwa hapo ulipo sasa.
MATUMIZI; JINSI UNAVYOWEZA KUDHIBITI MATUMIZI YAKO NA KUWA NA MAISHA BORA.
Jinsi ya kutambua matumizi muhimu na yasiyo muhimu.
Panga matumizi kabla hujapokea fedha unayotegemea.
Jinsi ya kudhibiti matumizi yako na bado ukawa na maisha bora.
Gharama zilizojificha ambazo zinaongeza matumizi yako.
Jinsi ya kuzuia matumizi kuongezeka pale kipato kinapoongezeka.
Jinsi ya kuepuka kurudishwa nyuma na utegemezi mkubwa.
MADENI; NAMNA YA KUONDOKA KWENYE MADENI NA KUEPUKA KUINGIA KWENYE MADENI MABAYA.
Madeni ni utumwa.
Madeni mazuri na madeni mabaya.
Jinsi ya kuondoka kwenye madeni.
Jinsi ya kuepuka kuingia kwenye madeni.
Kigezo muhimu cha kuzingatia pale unapofikiria kukopa.
BIASHARA; NJIA YA UHAKIKA YA KUTENGENEZA KIPATO KISICHO NA UKOMO.
Msingi muhimu wa biashara unaopaswa kuuelewa.
Kwa nini kila mtu anapaswa kuwa na biashara.
Kuanza biashara ukiwa chini kabisa.
Biashara unayoweza kuanza kufanya.
Mambo ya kuzingatia ili kukuza biashara yako.
UWEKEZAJI; NJIA YA KUIFANYA FEDHA IKUFANYIE WEWE KAZI, INGIZA KIPATO HATA KAMA UMELALA.
Maana ya uwekezaji na umuhimu wake kwenye uhuru wa kifedha.
Dhana ya COMPOUND INTEREST na RULE OF 72 na namna ya kuzitumia kufanikiwa kwenye uwekezaji.
Tofauti ya uwekezaji mzuri (ASSETS) na uwekezaji mbaya (LIABILITIES)
Aina tano kuu za uwekezaji unazopaswa kuzijua.
Jinsi ya kupangilia uwekezaji wako ili kuwa na uhuru wa kifedha.
Uwekezaji unaopaswa kuanza nao mara moja.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika uwekezaji ili kufanikiwa kifedha.
KODI; MISINGI YA KODI NA NJIA ZA KUPUNGUZA KODI.
Maana halisi ya kodi na umuhimu wake kwa maendeleo.
Kodi zinazokuhusu wewe moja kwa moja.
Jinsi unavyoweza kupata unafuu wa kodi.
BIMA; NJIA ZA KULINDA FEDHA NA MALI ZAKO.
Maana ya bima na umuhimu wake kwenye uhuru wa kifedha.
Bima unazopaswa kuwa nazo kwenye maisha yako.
Mambo muhimu ya kuzingatia unapochagua bima.
WATOTO; JINSI YA KUWAJENGEA WATOTO MSINGI MZURI WA KIFEDHA.
Umuhimu wa kuwajengea watoto msingi wa kifedha.
Umri sahihi wa kuanza kuwajengea watoto misingi ya kifedha.
Misingi ya kifedha ambayo unapaswa kuwajengea watoto wako.
Jinsi ya kuwafuatilia watoto kwenye elimu na misingi ya kifedha.
Kuwashirikisha watoto kwenye shughuli zako za kifedha.
KUTOA; MAISHA YA UTAJIRI YENYE MANUFAA KWA WENGINE.
Utajiri siyo kwa ajili yako mwenyewe, ni kwa ajili ya jamii.
Kuacha wosia na mgawanyo mzuri wa mali zako baada ya kifo chako.
Njia bora za kutoa utajiri wako kwa wengine.
Utoaji wa sadaka na mafungu mengine muhimu kulingana na imani yako.
Karibu sana rafiki yangu tujifunze pamoja kwenye semina hii nzuri na muhimu sana kwenye maisha yetu. Nakukumbusha rafiki, siku ni mbili pekee, baada ya tarehe 30/06/2017 hutapata nafasi ya kushiriki semina hii nzuri.
Hivyo kama bado hujajiunga, tuma ada yako leo, tsh 50,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717396253 kisha tuma ujumbe kwenye wasap namba 0717 396 253 na nitakuweka kwenye kundi la semina.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.
