KITABU; Socrates ’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 37 – 50.
Socrates alikuwa akishangaa sana jinsi gani watu hawapendi kufikiri.
Alisema watu wengi wanapenda kuamini kile walichopokea na wasikihoji.
Pale mtu anapojaribu kuhiji na kuona imani yake inatikiswa, anaacha kabisa kuhoji na kuchukua kufikiri.
Hilo linampelekea mtu kufanya kitu siyo kwa sababu anajua kwa nini anafanya, ila kwa sababu ndiyo amezoea kufanya.
Socrate anatufundisha kwamba ili kujua imani yetu hasa, ili kujua kwa nini tunafanya kile tunachofanya, tujiulize swali KWA NINI sana,
Kila unachofanya jiulize kwa nini, na kila jibu unalopataa jiulize tena kwa nini. Nenda na kwa nini hizo mpaka pale utakapokosa majibu kabisa.
Na hapo ndiyo utakuwa umepata kile kweli ambacho unaamini, kile ambacho kinakusukuma kufanya unachofanya.
Jiulize kwa nini unafanya kila unachofanya, na kika jibu jiulize kwa nini. Hata kama inakufanya utilie mashaka imani uliyonayo, wewe hoji, utaufikia ukweli na utakuweka huru.
Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa