KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 121 – 130.

Socrates aliamini rafiki mzuri ni yule ambaye mnaweza kukaa pamoja nakujadiliana, kujifunza na kupeana changamoto kuwa bora zaidi.
Katika enzi za Socrate, mji wa Anthens ulikuwa na utaratibu wa kuwa na mijadala ya jioni kwa watu mbalimbali.
Mijadala hii ilijulikana kama Symposium ambapo marafiki walikutana kwa pamoja, kula, kufurahi na kujadili kwa kina maswali mbalimbali na muhimu kwa ukuaji wao.

Hili ni jambo muhimu sana kufanya katika kuboresha mahusiano yetu. Kuwa na marafiki ambao mnaweza kujadili mambo magumu na muhimu ambayo yanamfanya kila mmoja kuchukua hatua.

Na siyo lazima marafiki hawa wawe watu unaofahamiana nao. Unaweza kuanza mazungumzo na watu usiowajua kabisa, muhimu ni kuuliza maswali mazuri na yenye kuonesha kujali.
Marafiki na wale wanaotuzunguka ni watu muhimu kwetu kukua katika falsafa.

Kocha Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa