If you desire to be good, begin by believing that you are wicked. – Epictetus
Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Tumepata nafasi nzuri na ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari ANZA KWA KUAMINI HUJAKAMILIKA…
Watu wengi wanapenda kuwa watu wema,
Wanapenda kuwatendea wengine wema,
Na kuwawezesha kuwa bora zaidi.
Lakini wengi wanakwama, kwa sababu wanaanza wakiamini wamekamilika.
Wengi wanapenda kuonekana hawana kasoro yoyote, kuona wapo kamili.
Na hapo sasa ndipo wanapojizuia kuweza kuwa wema na hata kuwa bora zaidi.
Kwa sababu mtu anapoamini kwamba tayari amekamilka, hawezi kukazana kuwa bora zaidi, anaona tayari amefika kileleni.
Lakini mtu anapoanza kwa kuamini na kukubali kwamba hajakamilika, kukubali kwamba ana mapungufu, anakuwa tayari kuyafanyia kazi na hili hupelekea yeye kuwa bora zaidi kila siku.
Ili kuwa bora zaidi, ili kuweza kuwa mwema kwa wengine, lazima ukubali hujakamilika, ukubali utakosea na uwe tayari kujiboresha zaidi.
Uwe na siku njema sana ya leo.
Rafiki na kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa