KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross.
UKURASA; 171 – 180.

Mpaka sasa umejifunza mambo mengi sana kuhusu mwanafalsafa Socrates.
Katika mengi uliyojifunza, yapo ambayo yanakuwa yamekuvutia na ambayo unaona yanaendana na wewe.
Mambo haya ndiyo yanaakisi Socrates ambaye yupo ndani ya kila mtu.
Kila mtu ana msukumo wa kufanya jambo sahihi kwake.
Kila mtu ana msukumo wa kuwa bora zaidi.
Na kila mtu ana msukumo wa kifanya mazuri kwa wengine.
Huyu ndiye Socrates aliyepo ndani ya kila mmoja wetu.
Jukumu lako ni kumwamsha Socrates huyu kwa kuweka kwenye matendo yale yote uliyojifunza.
Kila mtu anaweza kufanya na kuishi ile ndoto iliyopo ndani yake.
Kama atakuwa tayari kuisimamia na kuweka juhudi kubwa bila ya kukata tamaa.

Kocha Makirita Amani.
http://www.amkamtanzania.com/kurasa