Such as are your habitual thoughts, such also will be the character of your mind; for the soul is dyed by the thoughts. – Marcus Aurelius

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Ni nafasi nyingine nzuri sana na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UNACHOFIKIRI NDIYO UNACHOKUWA…
Tangu enzi na enzi, watu wamejifunza kitu kimoja kikubwa, kwamba kitu chenye nguvu sana kweye maisha yetu, ni mawazo yetu.
Yale mawazo yanayotawala akili zetu, ndiyo yanayotengeneza matendo na tabia zetu na hayo kutengeneza maisha yetu.

Mara nyingi watu wanafikiri wanaweza kubadili maisha yao kwa kubadili matendo yao, lakini hilo limekuwa halifanyi kazi, kwa sababu kama mawazo yanabaki vile yalivyo, hakuna kinachobadilika.

Wakati mwingine watu wanafikiri wapo huru kuishi watakavyo, kumbe wapo watu wanaotawala mwazo yao, wanaoamua nini wafikiri ambacho kitapelekea maisha yao kwenda kwa njia fulani.

Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vimekuwa vyombo vya propaganda, vyombo vya kutengenza ajenda ili kuendesha maisha ya watu kama baadhi ha watu wanavyotaka.
Huenda hapo ulipo, unafikiri unachofikiri kwa sabau ndiyo umeona kila mtu anakizungumzia kwenye mitandao ya kijamii, au vyombo vyote vya habari ndiyo vinazungumzia.
Mawazo ya aina hii hayawezi kukufikisha pale unapotaka wewe.

Unachohitaji ni kutengenza ajenda zao mwenyewe, kuwa na propaganda zako mwenyewe, kujitengenezea habari ambazo zinakufanya utawale mawazo yako kwa ndoto zako.
Kila wakati ufikiri kuhusu maisha yako na maono makubwa ya maisha yako.
Hii itatengeneza nguvu kubwa ya kukuwezesha kupiga hatua, kwa kujenga matendo yanayoendana na ndoto unazotaka kuzifikia.

Tawala akili yako kwa mawazo ya ndoto zako na wewe kuwa bora zaidi. Mengine nje ya hapo yape nafasi ndogo, lakini usikubali yatawale akili yako, utakuwa mtumwa kweye hayo.

Unakuwa kile unachofikiri, kama hutengenezi fikra zako mwenyewe, basi jua wapo watu wanakutengeneza kama watakavyo wao.

Nakutakia siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa