We have two ears and one mouth so that we can listen twice as much as we speak. – Epictetus

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari SIKILIZA ZAIDI…
Tunaishi kwenye zama ambazo kila mtu anataka kuongea, lakini hakuna aliye tayari kusikiliza.
Hata wakati mtu amenyamaza na mwingine anaongea, anakuwa hasikilizi bali anajipanga aongee nini, ajibu nini au apinge nini.
Kwa njia hii watu wamekuwa hatujifunzi, kwa sababu unapoongea hakuna kipya unachoingiza, unaendelea kurudia unachojua.

Tuna masikio mawili na mdomo mmoja kwa makusudi kabisa kwamba tunapaswa kusikiliza zaidi ya tunavyoongea.
Sikiliza mara mbili ya unavyoongea.
Na sikiliza siyo kwa nia ya kupata cha kujibu, au kwa nia ya kupinga, bali sikiliza kujifunza.

Ukisikiliza utajifunza, utajifunza zaidi ya unachojua sasa.
Nakutakia siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa