Because a thing seems difficult for you, do not think it impossible for anyone to accomplish. – Marcus Aurelius
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya nakubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUSHINDWA WEWE SIYO KUSHINDWA KILA MTU…
Wapo watu ambao wanaamini kama wao hawawezi basi kila mtu hawezi.
Wengine pia wanaamini kwa sababu wao wameshindwa, basi kila mtu lazima ashindwe.
Hawa ni watu sumu ambao unapaswa kukaa nao mbali, kwa sababu hawatakuachia kabisa upige hatua.
Watakuwa na kila namna ya kuhakikisha hupigi hayua, ili wao wasionekane ni wazembe.
Kwa upande wa pili sasa, tukija kwetu binafsi sasa,
Kushindwa sisi haimaanishi kila mtu atashindwa,
Kama sisi hatuwezi haimaanishi kila mtu hawezi.
Hivyo tuwape wengine nafasi ya kufanya,
Na tuwe tayari kujifunza kutoka kwa wengine walioweza kufanya yale tuliyoshindwa sisi.
Uwe na siku njema leo, uwe na utayari wa kujifunza kutoka kwa wengine.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa