Habari za leo rafiki yangu?

Ni matumaini yangu kwamba upo vizuri na unaendelea kuweka juhudi kubwa ili kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora sana. Hilo ndiyo jambo la msingi la kila mmoja wetu kufanya. Usiache kufanya hata kama changamoto ni nyingi.

Kila mwezi nimekuwa nakushirikisha kitabu cha kusoma, na nimekuwa nakupa mbinu ya kuweza kusoma kitabu kimoja kila mwezi hata kama huna muda kabisa. kupitia programu ya kusoma KURASA KUMI KILA SIKU za kitabu, utaweza kumaliza kusoma kitabu kimoja kila mwezi.

Ukisoma kitabu kimoja kila mwezi, ndani ya mwaka utakuwa umesoma vitabu 12, utakuwa mbali sana kuliko wengine wote.

Mwezi Novemba tunakwenda kusoma kitabu cha KANUNI ZA SIRI ZA MAFANIKIO kilichoandikwa na mwandishi Noah ST John.

secret code

Japokuwa kila kitu kuhusu mafanikio kipo wazi kabisa na kila mtu anaweza kujifunza na kujua, bado watu wengi wanaishi kinyume kabisa na kanuni za mafanikio. Wanaishi kwa kanuni ambazo haziwezi kabisa kuwaletea mafanikio kwenye maisha yao.

Na hili ndilo linafanya mafanikio kuonekana kama siri nzito, ambayo wachache pekee ndiyo wamefunuliwa huku wengi wakiteseka bila ya kuijua. Hapa ndipo mwandishi Noah alipoingilia kati na kuamua kutupa zile kanuni ambazo kila mtu akizifuata lazima atafanikiwa.

Noah anatupa hatua saba ambazo kila mtu akizifuata, ataweza kupata utajiri zaidi kwenye maisha yake na kuwa na furaha pia. Noah anaanza kitabu kwa kutuonesha namna ambavyo tumekuwa tunadanganywa na kuondolewa kwenye njia ya mafanikio.

Nisikumalizie utamu wa maarifa yaliyopo kwenye kitabu hichi, badala yake nikupe nafasi ya kujisomea kitabu hichi kwa mwezi huu wa Novemba.

Neno langu kwako rafiki yangu ni moja, soma kitabu hichi, kisome kama kweli upo makini na mafanikio yako kwenye maisha. Hichi siyo kitabu cha kuacha kusoma, kwa sababu kinakufungua na uone namna gani unapishana na mafanikio.

Je nakisomaje wakati sina muda kabisa?

Hapo ndipo pazuri, kwa sababu nimekuandalia program ya kusoma KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU. Kitabu hichi kina kurasa kama 250, ukisoma kurasa 10 kila siku, ndani ya siku 25 unakimaliza kabisa.

Program hii inaendeshwa kwa njia ya kundi la wasap, ambapo unaingia kwenye kundi hilo ambapo utapaswa kusoma kurasa kumi kila siku, kisha kuandaa muhtasari kidogo wa kurasa 10 ulizosoma, ulichojifunza na unachokwenda kufanyia kazi.

Kuingia kwenye kundi hili unapaswa kulipa ada ya mara moja ambayo ni tsh 10,000/=. Ukishalipa ada hii utakuwa kwenye kundi hili milele, kama utasoma kila siku. Lakini ikitokea umeshindwa kusoma kwa siku mbili mfululizo, utaondolewa kwenye kundi hili na ukitaka kujiunga utapaswa kulipa tena ada.

Haya ni marekebisho, awali ilikuwa ada ni elfu 10 kila mwezi, sasa ni elfu 10 mara moja pekee, ukikosa kusoma siku mbili mfululizo ndiyo utaondolewa na kuhitajika kulipa tena ada kama utapenda kujiunga. Hii inaitwa NEVER MISS TWICE.

Napata wapi kitabu hichi?

Utatumiwa kitabu hichi bure kabisa kwa njia ya softcopy ukishajiunga na program ya KUSOMA KURASA 10 ZA KITABU KILA SIKU. Kitabu utaweza kukisomea kwenye simu yako, kompyuta, tablet na kifaa kingine cha kielektroniki chenye uwezo wa kusoma vitabu.

Najiungaje na programu hiyo?

Unatuma ada, tsh 10,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA 0717 396 253 majina yatatokea Amani Makirita. Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na ujumbe wa KURASA KUMI ZA KITABU, utawekwa kwenye kundi na kupewa maelekezo zaidi.

Vitabu

Nimekuwa nasema hili rafiki, kama unajua kusoma lakini husomi, huwezi kumcheka asiyejua kusoma, kwa sababu wote mnakosa fursa sawa. Kwa mfano sasa hivi wewe unaweza kuwa unakazana kufanya kazi na biashara zako, kwa njia ambayo inakuzuia kufanikiwa. Lakini ukisoma kitabu hichi cha kanuni za mafanikio, utaona wapi unakosea na kuweza kurekebisha.

Karibu sana kwenye program ya kusoma KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU, ujifunze kupitia kusoma vitabu na kupitia wengine pia.

Fanya malipo sasa na tuungane pamoja.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog