KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 47 – 56.
Kitu kikubwa ambacho kilimwezesha Leonardo da Vinci kufanya makubwa kwenye maisha yake ni udadisi.
Tangu akiwa mdogo alikuwa akihoji mambo mbalimbali. Kila alichokiona alihoji na kutaka kujua zaidi. Hilo lilimpelekea yeye kujifunza na kusoma zaidi ili kuweza kupata majibu sahihi.
Nguvu hii ya udadisi kila mtu amewahi kuwa nayo. Hasa kwa umri wa utoto na wakati wa ukuaji, watu huhoji mambo mengi sana. Lakini kwa kuwa wazazi wanakuwa hawana majibu sahihi, huwazuia watoto kuhoji.
Ili uweze kutoka hapo ulipo sasa,
Ili uweze kupiga hatua,
Ili uweze kuujua ukweli kama ulivyo,
Lazima uwe mtu wa kuhoji.
Hupaswi kuwa mtu wa kukubaliana na kile ambacho kila mtu anakubaliana nacho au anafanya.
Unahitaji udadisi, unahitaji kuhoji, kujifunza zaidi ili uweze kupata majibu sahihi.
Amsha nguvu ya udadisi iliyopo ndani yako,
Hoji na dadisi kila kitu ili uweze kupata majibu sahihi na kupiga hatua.
Usihoji tu kujifurrahisha, au kuhoji ili kuwakwamisha wengine, bali hoji ili kuchukua hatua na kuwa bora zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa