KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 104 – 113.
Tunaishi kwenye zama ambazo watu wanapenda kuwa na uhakika wa kile wanachofanya. Lakini hili halikuwa hivyo wakati wa Leonardo da Vinci.
Katika kipindi hicho, ilikuwa ni muhimu kuweza kuvumilia hali ya kutokuwa na uhakika.
Kuweza kuishi na hali ya kutokuwa na uhakika kilikuwa kipimo kizuri cha maisha bora, hasa kwa wanafalsafa na viongozi.
Moja ya vitu vinavyoashiria uwezo wa Leornado kukubali hali ya kutokuwa na uhakika ni mchoro wake wa picha ya Monalisa. Ni picha ambayo imezua mijadala kwa wengi kwa sababu haijulikani kwa hakika ni nani aliyechorwa kwenye picha ila.
Imekuwa ina tafsiri nyingi kwa watu mbalimbali.
Na mwisho wa siku watu wamekubali kwamba hakuna mwenye uhakika, huenda hata Leornado mwenyewe hakuwa na uhakika.
Kuna mambo mengi sana kwenye maisha yetu ambayo hatuna uhakika nauo, lakini lazima tuyafanye. Uthubutu wetu wa kufanya mambo hayo ni kitu cha kwanza kututenganisha na wengine ambao wanaahindwa kupiga hatua.
Tuwe na uthubutu, tukubali hali ya kutokuwa na uhakika, na tuchukue hatua kusonga mbele zaidi.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa