KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb
UKURASA; 114 – 123.

Moja ya vitu vilivyomwezesha Leornado kuwa na umaarufu mkubwa ni mawazo bora kabisa aliyokuwa anakuja nayo. Mengi yalikuwa ni mawazo ambayo alikuwa akiyapata akiwa amepumzika au akiwa anafanya kitu ambacho hakimchoshi au kuumiza akili.

Hata ukifuatilia maisha ya watu wengine ambao waliweza kuja na mawazo bora, wengi walipata mawazo hayo wakiwa wamepumzika au wakifanya mambo ambayo siyo kazi kubwa.
Wapo waliopata mawazo bora wakiwa wanatembea, wengine wakiwa wanaoga, wengine wamelala na pia wapo waliopata mawazo bora wakiwa wanatahajudi.

Ili kuiruhusu akili yako kuweza kuja na mawazo bora kabisa, ipe muda wa kupumzika. Ipe akili yako muda wa kufikiri na kufanya mambo mengine, nje kabisa ya shughuli zako za kila siku.
Hapo utashangaa unapata majibu ya changamoto ambazo umeshasumbuka nazo kwa muda mrefu.

Unapokuwa na changamoto kubwa unayotaka kutatua, au unahitaji mawazo bora, jipe muda wa kuwa nje ya kazi au biashara yako. Hapo unaweza kutembea, kulala, kutahajudi na hata kukaa bila ya kufanya chochote.
Katika hali kama hii, akili yako inapata mawazo bora kabisa kwako.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kurasa