Each day provides its own gifts. – Marcus Aurelius
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Ni siku nyingine nzuri sana kwetu ambapo tumepata nafasi ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari ZAWADI YA LEO…
Kila siku mpya kwenye maisha yako ni zawadi kubwa kwako. Ni nafasi ya wewe kufanya kile ambacho ni muhimu zaidi kwako.
Kila siku unayoianza ina zawadi yake, kuna kitu cha kipekee unachoweza kufanya au kupata na kikaifanya siku hiyo kuwa ya tofauti kwenye maisha yako.
Hivyo basi rafiki yangu, kwa leo na kila siku ya maisha yako, ichukulie kama zawadi ambayo hutaipata tena, na kwa hakika hutaipata tena siku hii ya leo.
Pia unavyoiendea siku yako, tafuta zawadi yako ya siku hiyo.
Kwa kuwa tunapata kile tunachotafuta, ukitafuta zawadi yako ndani ya siku yako, utaipata.
Chukua zawadi yako ya siku ya leo, na nenda kaitafute zawadi iliyopo ndani ya siku hii.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha