Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kuwa tunayapenda kwenye maisha yetu, lakini kwa hali tunayokuwa nayo kwa wakati huo, tunaona hatuwezi kuyamudu. Na hivyo tunaamua kusubiri ili tuweze kuyamudu mambo hayo. Na hapo sasa ndipo tunapojichelewesha kwa kiasi kikubwa sana.

Ni vigumu sana kuweza kumudu kila kitu ambacho mtu unakitaka kwenye maisha yako, hasa kwa wakati ambao unakitaka. Lakini kusubiri mpaka uweze kukimudu pia siyo mpango mzuri, kwa sababu vitu vingi havisubiri.

Achana

Hivyo njia bora kabisa kwa vile vitu ambavyo mtu huwezi kuvimudu, ni kuanza kuvifanya kwa hatua ndogo, kuanza kwa kiasi kidogo sana ambacho hakihitaji rasilimali kubwa na nyingi.

SOMA; UKURASA WA 823; Chagua Unamalizaje….

Kwa chochote unachofikiria kufanya lakini unaona huwezi kukimudu au hujawa tayari, angalia wapi unapoweza kuanzia kisha anza. Muhimu zaidi ni kuanza, maana hata kama unahitaji msaada wa wengine, watakuwa tayari kukusaidia wakikuona unafanya kuliko ukiwa mtu wa kuongea pekee.

Pia unapofanya, unaziona fursa nyingine za kupiga hatua zaidi, ambazo huwezi kuziona kama hujaingia na kufanya.

Usisubiri mpaka uweze kumudu chochote unachotaka kufanya. Angalia wapi unapoweza kuanzia kisha anzia hapo, mengine yatajipanga vizuri kadiri muda unavyokwenda.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog