Habari za leo rafiki yangu?

Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, ambapo tumepata nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Twende tukaitumie siku hii vizuri ili tuweze kuweka alama ya tofauti kwenye maisha yetu na ya wengine pia.

Leo nataka nikushirikishe maajabu niliyoyagundua kuhusu mwaka 2018, ambayo yananishangaza na yanaweza kukushangaza pia.

Nilichogundua ni kwamba, mwaka 2018 hauna mwezi Januari, ndiyo yaani mwezi wa kwanza haupo kabisa. Mwezi huu haupo kwenye mawazo wala mipango ya wengi, na hapo ndipo tatizo kubwa linapoanzia.

Angalia rafiki, kila mwaka, mwezi Januari umekuwa unalaumiwa na watu walio wengi. Kila mtu utamsikia akisema Januari ngumu kweli. Wengine wanasema Januari ndiyo mwezi mrefu kuliko miezi mingine yote. Na maneno mengine ambayo watu wamekuwa wakijifariji nayo.

Kinachoshangaza ni kwamba, kila mwisho wa mwaka huwa kuna sikukuu na sherehe nyingi, ambazo watu hushiriki kwa njia mbalimbali. Sikukuu na sherehe hizi zinatumia gharama, ambazo watu hujiandaa vyema na kuhakikisha zinakwenda vizuri.

Lakini wakati wakifurahia sikukuu hizo, ni kama vile hawajui mwezi unaofuata ni mwezi Januari, mwezi ambao maisha lazima yaendelee tena, tena kwa majukumu mengi na makubwa.

Kila mtu anajua kwamba mwezi Januari una majukumu makubwa kwa wengi, ni mwezi ambao shule zinafunguliwa na hivyo ada na mahitaji ya kielimu yanahitajika. Ni kipindi ambacho malipo mbalimbali yanahitajika kufanyia kama kodi za nyumba. Na pia ni kipindi ambacho baadhi ya maeneo msimu wa kilimo ndiyo unaanza, hivyo maandalizi ya kilimo kuhitajika.

Lakini pamoja na yote hayo, watu husahau kabisa kuhusu mwezi Januari na kula maisha mwezi Disemba. Hii ndiyo sababu nashawishika kuamini kwamba, kwenye akili na mawazo ya wengi, mwezi Januari haupo, mpaka pale unapofika ndiyo watu wanapatwa na butwaa. Yaani tunaweza kusema kwamba, mwezi Januari kwa sasa haupo ila utakuja kwa ‘surprise’. Yaani ghafla Januari hii hapa, na haiishi kabisa.

Hivyo wito wangu kwako rafiki yangu, usiwe kama wengi ambao wanajisahaulisha kuhusu uwepo wa mwezi januari. Usiwe kati ya wale ambao mwezi huu wa disemba unakula maisha ukiwa umesahau kabisa kwamba mwezi unaofuata una majukumu mengi.

Badala yake kuwa na mipango ya miezi yote inayofuata ya maisha yako. Jua majukumu na mahitaji yako ni yapi na kila hatua unazochukua sasa jua kwamba kuna maisha baada ya kila unachofanya.

Unapofurahia na kusherekea sherehe za mwisho wa mwaka kumbuka kuna mwezi unaofuata, mwezi wenye mahitaji makubwa.

Mwisho kabisa usikubali kuwa mmoja wa watu wanaolalamikia mwezi, kusema mwezi ni mgumu au mwezi ni mrefu au mwezi ni dume. Badala yake kuwa na mipango kwa kila hatua unazochukua na kwa kila majukumu yaliyopo mbele yako.

KWA NINI SIYO TAJIRI

Karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018 kwa mafanikio.

Kila mwaka, mwanzoni nimekuwa nakushirikisha namna bora ya kubadilika, jinsi ya kujenga mifumo mizuri ya maisha ambayo itakuwezesha kufanikiwa kila siku na kwa mwaka mzima.

Kwa mwaka huu mpya tunaouendea wa 2018, nimekuandalia semina ya siku 5 itakayoendesha kwa njia ya mtandao. Semina hii itaendeshwa kwenye mtandao wa WASAP ndani ya kundi la KISIMA CHA MAARIFA, kundi ambalo kwa mwaka mzima unaendelea kujifunza kila siku.

Mada za semina.

Kwenye semina hii ya kuuanza mwaka 2018, tutajifunza mambo yafuatayo;

Siku ya kwanza; karibu mwaka mpya, jitengeneze wewe kuwa mpya.

Siku ya pili; maneno matatu ya kutuongoza kwa mwaka 2018.

Siku ya tatu; mfumo bora wa siku na maisha ya mafanikio.

Siku ya nne; fedha na uwekezaji kwa mwaka 2018

Siku ya tano; hatua za kwenye kazi, biashara na mahusiano kwa mwaka 2018.

Kwa siku hizo tano tutajifunza kwa kina na kila mmoja wetu kuondoka na mpango wa kuishi na kufanyia kazi kwa mwaka 2018. Mpango ambao utazuia changamoto au matatizo kuwa kikwazo kwetu kupata kile tunachotaka.

Tarehe ya kufanyika kwa semina.

Semina itafanyika kwa siku tano, kuanzia jumatatu ya tarehe 08/01/2018 mpaka ijumaa ya tarehe 12/01/2018.

Jinsi ya kushiriki semina hii.

Ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama, hakuna gharama za ziada za kulipa ili kushiriki semina.

Kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= (elfu hamsini). Hii ni ada ya mwaka mzima, kwa kipindi cha miezi 12 tangu unapojiunga.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unaendelea kujifunza mengine mengi kila siku, ikiwa ni pamoja na kushiriki semina nyingine ya njia ya mtandao na semina ya kuhudhuria pia.

Jinsi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Unalipa ada tsh 50,000/= kwa njia ya simu; MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 Namba hizo zina jina AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwenye moja ya namba hizo kisha utaunganishwa kwenye kundi la WASAP.

Mwisho wa kujiunga ili kushiriki semina.

Japokuwa kujiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni muda wowote mtu unaotaka, ili unufaike na semina hii, ni muhimu ujiunge kabla haijaanza, ili uweze kushiriki somo la kwanza mpaka la mwisho.

Hivyo tarehe ya mwisho ya kujiunga ili kushiriki semina hii itakuwa ijumaa ya tarehe 05/01/2018.

Karibu sana tuuanze na kuenda na mwaka 2018 kwa pamoja, tuweze kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog