Kila mtu anaweza kutamani,

Unamwona mtu ana kitu fulani ambacho na wewe ungependa kuwa nacho, unakitamani, na kufikiria na wewe pia unaweza kuwa nacho. Hii ni hatua ya kwanza kabisa kwenye mafanikio na hata mipango yetu. Lazima kuwe na kitu cha kutufanya tuone tunataka zaidi ya tulichonacho sasa.

Wapo watu ambao wanajua nini wanataka, wanapanga kabisa kwamba wanataka kufika wapi, wanajua nini wanapaswa kufanya na wakati gani ili kupata kile wanachotaka. Kutaka siyo kugumu sana, kwa sababu wengi wanaweza kuweka mipango yao.

Kila Changamoto

Kuna kitu ambacho kinawatofautisha wachache wanaopiga hatua kubwa kwenye maisha yao na wale wengi ambao wanaishia kutamani na kutaka. Kitu hicho ni kujitoa. Hii ni hatua ambapo mtu anafanya kila anachopaswa kufanya kuhakikisha anapata kile anachotaka.

Kwa aliyejitoa, hakuna chochote kinachoweza kumzuia kupata anachotaka, hakuna cha kumrudisha nyuma, anakuwa amejitoa kweli, na anapata kile anachotaka.

Siyo kwamba hakutani na vikwazo au changamoto, na siyo kwamba hana hofu ya kushindwa ndani yake, vyote hivyo anavyo, lakini vinazidiwa nguvu na kule kujitoa ambapo mtu anakuwa amefikia.

Anakuwa hana namna nyingine bali kupata kile anachotaka, anakuwa mbishi na king’ang’anizi mpaka dunia inampisha apate kile anachotaka.

SOMA; UKURASA WA 1043; Kufanya Kazi Kwa Nguvu, Akili, Kujitoa Na Kuamini Unachofanya.

Sitaki kukuuliza kuhusu kutamani wala kutaka, ninachotaka ujiulize je ni vitu gani umejitoa kuvipata au kuvifikia kwenye maisha yako? Ni kwa yapi hakuna yeyote anayeweza kuurudisha nyuma?

Kama huna mambo ambayo umejitoa kwa kuyapata na kuyafikia, nafasi za mafanikio zinakuwa finyu sana kwa dunia hii yenye ushindani na changamoto za kila aina.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog