It’s not because things are difficult that we dare not venture. It’s because we dare not venture that they are difficult. – Lucius Annaeus Seneca
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari; SIYO UGUMU WA VITU, NI UGUMU WETU WENYEWE…
Kuna wakati tunajiaminisha kwamba hatuwezi kufanya baadhi ya vitu fulani kwa sababu ni vigumu.
Tunakuwa tumeacha kufanya kwa kuwa tunaona ni vigumu.
Lakini huo siyo ukweli,
Siyo kweli kwamba tunashindwa kufanya vitu kwa sababu ni vigumu.
Ukweli ni kwamba vitu ni vigumu kwa sababu hayujadhubutu kuvifanya.
Chochote ambacho hujawahi kufanya, lazima kitaonekana kigumu kwako.
Lakini pale unapochukua hatua na kuanza kufanya, unaanza kuona kumbe ni vitu vya kawaida, kumbe inawezekana kufanyika.
Kitu hata kama kinaonekana ni kigumu kiasi gani, unapoanza kupiga hatua kwenye kukifanya, unaona njia na fursa zaidi za kufanya kwa ubora zaidi.
Hivyo moja ya jambo ya kufanya mwaka huu 2018, ni kuchukua hatua na kuanza kufanya yale mambo ambayo umekuwa unaona ni magumu.
Anza kuyafanya kwa hatua ndogo, na kuwa na mtazamo wa kujifunza.
Utaziona njia bora kabisa za kufanya.
Ugumu tunaitengeneza wenyewe, anza kuuvunja sasa.
Ukawe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha