Habari za leo rafiki?

Moja ya vitu ambavyo kila mtu hujikuta anafanya mwanzoni mwa mwaka hata kama hajui kwa nini anafanya, ni kuweka malengo. Kila mtu huwa na kitu cha kusema wakati mwaka unaanza. Wapo wanaosema mwaka mpya mambo mapya, wengine wakiamini mwaka mpya utakuwa na mabadiliko makubwa kwenye maisha yao.

Lakini mwezi mmoja unapoisha baada ya mwaka kuanza, sehemu kubwa ya watu wanakuwa wameshasahau yale malengo waliyojiwekea, wanakuwa wamesharudi kwenye maisha yao ya zamani na wanasubiri tena mwaka unaokuja warudie zoezi hilo la kujifariji.

Baada ya kuona changamoto hii kwangu binafsi na kwa wengine pia, ndipo niliona umuhimu wa kuwa na kitu cha tofauti ambacho kitawasaidia watu kufikia malengo wanayojiwekea.

Katika kufanya tafiti na kujaribu njia mbalimbali, nimegundua aina za malengo ambazo watu wanajifurahisha kuweka, ambayo kwa namna yoyote ile hayawezi kufikiwa.

Ndiyo maana hapa nakuambia, kuna aina ya malengo kama umeyaweka, basi jua tu umejifurahisha, hutayafikia na baada ya muda utarudi kwenye hali yako ya kawaida.

malengo ya 2018

Mfano wa malengo ambayo watu wanajiwekea ambayo hawawezi kuyafikia;

‘Mwaka huu 2018 ni mwaka wangu wa kupata fedha nyingi zaidi’

‘Mwaka huu 2018 nitajenga’

‘Mwaka huu 2018 nitaandika kitabu’

‘Mwaka huu 2018 nitasoma vitabu zaidi’

‘Mwaka huu 2018 nitanunua gari’

Nafikiri unaona huo mtiririko jinsi unavyokwenda. Utaona jinsi ambavyo malengo hayo yamekaa kuwa ya kutaka kupata kitu, lakini hayana eneo la kile ambacho mtu unatoa ili kupata unachotaka.

Huwa tunaamini mwaka mpya ndiyo unaleta vitu, kama vile mwaka una nguvu yoyote ya tofauti kwa mtu.

Lakini ukweli ni kwamba, mwaka mpya ni mabadiliko tu ya tarehe, kila kitu kwenye mwaka mpya ni kile kile, mpaka pale wewe binafsi utakapochagua kubadili chochote unachotaka kiwe tofauti. Na mabadiliko haya, huwa yanaanzia ndani yako mwenyewe ndipo yanatokea kwenye vitu.

Swali ni je malengo ya aina gani ambayo yanafikika? Ni malengo gani ukiyaweka utaweza kuyafikia?

Na jibu ni moja, malengo ambayo yamejengewa mfumo, malengo ambayo yanaanza na mabadiliko ndani yako, kwa kubadili mfumo wako w amaisha na namna unavyofanya vitu ndivyo unayoweza kuyafikia.

Kwa mfano kusema mwaka huu nitaandika kitabu, hakuna nguvu kubwa, unaweza kuahirisha kadiri utakavyo, ukiamini bado mwaka haujaisha na utaandika kitabu. Lakini lengo hili hili ukalibadili na kutengeneza mfumo, mfumo wa kuandika kila siku maneno 500, utalifikia kwa urahisi zaidi bila hata ya kushawishika kuahirisha. Wewe unachofanya ni kuandika maneno 500 kila siku na ndani ya miezi mitatu utakuwa umeshakamilisha kitabu chako.

Kadhalika kwenye kuweka akiba na kuwekeza, kusema utaweka akiba hakukusukumi sana kuchukua hatua. Lakini ukiweka mfumo kwamba kila asilimia 10 ya kipato unachopata moja kwa moja inaenda kwenye akiba, ni kitu kinachotekelezeka na kitakuwezesha kufikia lengo hilo.

Kinachokosekana

Ni nidhamu ya kufuata mfumo ndiyo inayowasumbua na kuwakwamisha wengi, na ndiyo maana nimekuandalia kitu kizuri sana kitakachokuwezesha wewe kuchukua hatua kubwa kwa mwaka huu 2018.

Nimekuandalia semina ya kipekee ya kuuanza mwaka 2018 kwa mafanikio makubwa sana ambayo yanaanzia ndani yako mwenyewe.

Hii ni semina ambayo inafanyika mara moja tu na hupaswi kuikosa kama unapenda kupiga hatua na kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.

Semina hii itakuwa ya siku tano na itaendeshwa kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani, na kwa muda wako binafsi. Huhitaji kusafiri kwenda popote na huhitaji kuacha kazi zako ili kushiriki. Ni wewe kuhakikisha upo kwenye kundi na kufuatilia mafunzo kadiri ya muda wako.

Mada za semina.

Kwenye semina hii ya kuuanza mwaka 2018, tutajifunza mambo yafuatayo;

Siku ya kwanza; karibu mwaka mpya, jitengeneze wewe kuwa mpya.

Siku ya pili; maneno matatu ya kutuongoza kwa mwaka 2018.

Siku ya tatu; mfumo bora wa siku na maisha ya mafanikio.

Siku ya nne; fedha na uwekezaji kwa mwaka 2018

Siku ya tano; hatua za kwenye kazi, biashara na mahusiano kwa mwaka 2018.

Kwa siku hizo tano tutajifunza kwa kina na kila mmoja wetu kuondoka na mpango wa kuishi na kufanyia kazi kwa mwaka 2018. Mpango ambao utazuia changamoto au matatizo kuwa kikwazo kwetu kupata kile tunachotaka.

Tarehe ya kufanyika kwa semina.

Semina itafanyika kwa siku tano, kuanzia jumatatu ya tarehe 08/01/2018 mpaka ijumaa ya tarehe 12/01/2018.

Jinsi ya kushiriki semina hii.

Ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama, hakuna gharama za ziada za kulipa ili kushiriki semina.

Kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= (elfu hamsini). Hii ni ada ya mwaka mzima, kwa kipindi cha miezi 12 tangu unapojiunga.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unaendelea kujifunza mengine mengi kila siku, ikiwa ni pamoja na kushiriki semina nyingine ya njia ya mtandao na semina ya kuhudhuria pia.

Jinsi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Unalipa ada tsh 50,000/= kwa njia ya simu; MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 Namba hizo zina jina AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwenye moja ya namba hizo kisha utaunganishwa kwenye kundi la WASAP.

Mwisho wa kujiunga ili kushiriki semina.

Japokuwa kujiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni muda wowote mtu unaotaka, ili unufaike na semina hii, ni muhimu ujiunge kabla haijaanza, ili uweze kushiriki somo la kwanza mpaka la mwisho.

Hivyo ni muhimu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 07/01/2018 ili uweze kujiandaa vyema na masomo haya ya semina.

Karibu sana tuuanze na kuenda na mwaka 2018 kwa pamoja, tuweze kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog