In war there is no prize for runner-up. – Lucius Annaeus Seneca
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nzuri na ya kipekee sana ya leo.
Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari; ZAWADI YA MSHINDI WA PILI…
Kwenye mashindano mbalimbali ambayo watu huwa wanashiriki, kuna zawadi ya mshindi wa kwanza, mshindi wa pili na mpaka mahindi wa tatu.
Kwa kuzoea hili kwenye michezo na mashindano mbalimbali, tunaweza kufikiri kwamba kila kitu kwenye maisha kinapaswa kuwa na zawadi kwa kila mshiriki.
Lakini kuna vitu ambavyo havina utaratibu huo wa zawadi kwa washiriki wengi.
Ni labda umeshinda, au umeshindwa, hakuna mshindi wa pili na kuendelea.
Vitu hivyo ambavyo hakuna mahindi wa pili ni Vita na maisha kwa ujumla.
Kwenye vita yoyote, kuna upande ambao utashinda, na upande ambao utashindwa, hakuna mshindi wa pili.
Kadhalika kwenye maisha yako, ni unakazana ufikie ndoto zako au usizifikie, hakuna ushindi wa pili.
Kwa kujua hili kwamba yapo maeneo ambayo hayana ushindi wa pili, unajitoa kweli kweli kuhakikisha unaweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Na pale unaposhindwa kupata matokeo hayo, unajipanga vizuri zaidi na kuweka juhudi kubwa zaidi ili kupata matokeo bora.
Usijipe ushindi wa pili ambao haupo.
Pambana ushinde, na usiposhinda jifunze ili uweze kushinda wakati mwingine.
Ukawe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha