Rafiki,

Kuna watu waliweka malengo makubwa ya mwaka 2018 siku ya tarehe 01/01/2018, wakiwa na hamasa kubwa na kujiona tayari wameshapata mafanikio makubwa sana.

Lakini leo tarehe 04/01/2018, wanaamka wakijiuliza hivi yale waliyojiambia watafanya 2018 yanawezekana kweli? Hivi yale makubwa waliyojiahidi yapo ndani ya uwezo wao kweli? Unapanga kuanza kufanya lakini wakati halisi wa kufanya unakutana na sababu za kukufanya uahirishe kufanya.

Hali hii hutokea kwa karibu watu wote wanaoweka malengo na mipango ya kila mwaka mpya. Kuna ambao hali hii inawatokea ndani ya wiki moja, wengine wiki mbili. Lakini wengi huwa wanakuwa wameshaachana na malengo moja wiki tatu mpaka mwezi baada ya mwaka kuanza.

Ili hili lisitokee kwako rafiki yangu, nimekuandalia hatua tano muhimu za kuchukua kwa siku tano ili mwaka huu 2017 uwe wa mafanikio makubwa kwako.

Nimekuandalia semina ya siku tano kwa njia ya mtandao, ambapo utakwenda kujifunza mambo matano muhimu sana ya kuufanya mwaka huu kuwa bora kwako.

2018 best year ever

Mambo hayo matano yatakayofanyika kwa siku tano ni kama ifuatavyo;

Siku ya kwanza; karibu mwaka mpya, jitengeneze wewe kuwa mpya.

Watu wengi wamekuwa wakifurahia upya wa mwaka, lakini wao wanaendelea kuwa vile vile. Sasa haijalishi unataka mafanikio kiasi gani, haijalishi una hamasa kiasi gani, kama wewe hutabadilika, basi hakuna kitakachobadilika.

Lakini mabadiliko ni magumu, ni machungu na yanaumiza na kuibua hofu. Kwenye siku ya kwanza kabisa ya semina hii, nitakwenda kukushirikisha njia ya uhakika ya kuyafanya mabadiliko kuwa bora kwako. Njia hiyo itakufanya ubadilike wewe kuanzia ndani yako, na usirudishwe nyuma.

Ukikosa hatua hii ya kwanza na muhimu, kuwa na uhakika kwamba mwaka 2018 umechagua kuupoteza.

Siku ya pili; maneno matatu ya kutuongoza kwa mwaka 2018.

Mwaka 2015 mwishoni nilijifunza dhana ya kuwa na maneno matatu muhimu ya kukuongoza kwa mwaka mzima. Hivyo mwaka 2016 nilitafakari kwa kina na kupata maneno matatu ambayo yalikuwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA. Maneno haya matatu yalisababisha mabadiliko na mafanikio makubwa kwangu na kwa wanachama wengi wa KISIMA CHA MAARIFA kitu kilichonifanya niyachague kuwa maneno matatu ya msingi wa maisha ya mafanikio, na tunaendelea nayo mpaka sasa.

Mwaka 2017 tulikuwa na maneno matatu, KUTHUBUTU, USHINDI, SHUKRANI, ni maneno ambayo yametuwezesha kuthubutu na kushinda zaidi 2017, muhimu zaidi, tumeweza kuwa na shukrani kwa kila jambo.

Mwaka huu 2018 nimekuandalia maneno matatu ambayo kwa kuyaishi hayo, utaweza kupiga hatua kubwa sana 2018. Karibu sana kwenye semina uyapate na kuyaishi maneno haya.

Siku ya tatu; mfumo bora wa siku na maisha ya mafanikio.

Watu wamekuwa wanakosea kitu kimoja wanapoweka malengo, wanaangalia pale wanapotaka kufika, halafu wanaanza kukazana kujaribu vitu ambavyo vinaweza kuwafikisha pale. Kwa njia hii wanakosa mfumo mzuri wa kufika pale wanapotaka kufika.

Ipo hivi rafiki, mafanikio yoyote ni matokeo ya hatua ndogo ndogo ambazo mtu anakuwa anachukua kila siku. Hivyo moja ya vitu unapaswa kufanya mwaka 2018 ni kuwa na utaratibu wa maisha yako ya kila siku.

Unahitaji mfumo wa kuiishi kila siku ya mwaka huu 2018, unahitaji kuwa na mambo ambayo unayafanya kila siku na kwa muda fulani wa siku yako, ili uwe kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa.

Utajifunza hili kwa kina kwenye semina ya siku tano, na utaweza kuiishi kila siku ya mwaka 2018 kama siku ya mafanikio makubwa.

Siku ya nne; fedha na uwekezaji kwa mwaka 2018

Kitu kinachoongoza kuwanyima watu usingizi ni fedha, hata wale wanaosema fedha siyo muhimu, fedha ndiyo imetawala mawazo yao.

Hivyo kuna mambo muhimu sana ambayo kila mtu anapaswa kuyazingatia linapokuja swala la fedha. Na kwa mwaka huu 2018, kuna mambo muhimu sana ya kuyajua na kuyafanyia kazi kuhusu eneo la fedha.

Watu wamekuwa wanafanya makosa sana kwenye fedha, hata wakikazana kuongeza kipato, ndiyo wanazidi kujikuta kwenye madeni zaidi.

Karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018 ujiweke vizuri kwenye eneo la fedha.

Siku ya tano; hatua za kuchukua kwenye kazi, biashara na mahusiano kwa mwaka 2018.

Mwisho kabisa, kuna hatua muhimu sana ambazo unapaswa kuchukua kwenye kazi yako, biashara na hata mahusiano yako. Haya ni maeneo muhimu sana ambayo wengi huwa wanayaendesha kwa mazoea na wanajikuta wakipata changamoto kila wakati.

Kwenye siku ya tano ya semina, tutakwenda kuangalia hatua muhimu za kuchukua kwenye maeneo haya muhimu ili kuweza kupata matokeo bora.

Kwa siku hizo tano tutajifunza kwa kina na kila mmoja wetu kuondoka na mpango wa kuishi na kufanyia kazi kwa mwaka 2018. Mpango ambao utazuia changamoto au matatizo kuwa kikwazo kwetu kupata kile tunachotaka.

Karibu sana kwenye siku hizi tano za semina, ambayo itafanyika kwa njia ya mtandao wa wasap, kwenye Kundi la KISIMA CHA MAARIFA.

Tarehe ya kufanyika kwa semina.

Semina itafanyika kwa siku tano, kuanzia jumatatu ya tarehe 08/01/2018 mpaka ijumaa ya tarehe 12/01/2018.

Jinsi ya kushiriki semina hii.

Ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama, hakuna gharama za ziada za kulipa ili kushiriki semina.

Kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh 50,000/= (elfu hamsini). Hii ni ada ya mwaka mzima, kwa kipindi cha miezi 12 tangu unapojiunga.

Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unaendelea kujifunza mengine mengi kila siku, ikiwa ni pamoja na kushiriki semina nyingine ya njia ya mtandao na semina ya kuhudhuria pia.

Jinsi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Unalipa ada tsh 50,000/= kwa njia ya simu; MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 Namba hizo zina jina AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwenye moja ya namba hizo kisha utaunganishwa kwenye kundi la WASAP.

Mwisho wa kujiunga ili kushiriki semina.

Japokuwa kujiunga na kundi la KISIMA CHA MAARIFA ni muda wowote mtu unaotaka, ili unufaike na semina hii, ni muhimu ujiunge kabla haijaanza, ili uweze kushiriki somo la kwanza mpaka la mwisho.

Hivyo ni muhimu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 07/01/2018 ili uweze kujiandaa vyema na masomo haya ya semina.

Karibu sana tuuanze na kuenda na mwaka 2018 kwa pamoja, tuweze kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye semina ya kuuanza mwaka 2018.

MUHIMU; NAFASI ZINAZOPATIKANA NA KUSHIRIKI NI CHACHE.

Siku chache zilizopita nilikushirikisha kwamba kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA limeshajaa, kwa kufika idadi ya mwisho inayoruhusiwa ya watu kuwa kwenye kundi la wasap. Na nilikuambia sitaweza kufungua kundi la pili, hivyo nitakupa taarifa pale zitakapopatikana nafasi.

Mwanzo huu wa mwaka zimepatikana nafasi chache ambazo naona unaweza kuzifaidi wewe rafiki yangu. Hivyo kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, chukua hatua leo hii ili usikose nafasi hii bora na ya kipekee kabisa ya kuufanya mwaka 2018 kuwa mwaka bora sana kwako.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA LEO, lipa ada, tsh 50,000/= kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe kwa wasap 0717 396 253 wenye majina yako na nitakuunganisha kwenye kundi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,