Zama za taarifa, zama za teknolojia ambazo tumeungana kwa masaa 24. Sasa hizi, kwa masaa 24 ya siku unaweza kupata taarifa yoyote unayotaka, unaweza kuwasiliana na yeyote unayetaka.

Muunganiko huu unaweza kuwa kitu kizuri, na unaweza kiwa kitu kibaya pia, kama hutaweza kuutumia vizuri.

Kwa mfano, kadiri watu wanavyounganika na wengine, ndiyo wanavyojitenga na wao wenyewe. Kadiri inavyokuwa rahisi kwa watu kukufikia wewe kwa masaa 24 ya siku, ndivyo inavyokuwa vigumu kwako kuungana na wewe binafsi.

disconnected

Sasa hivi ni mara chache sana mtu anaweza kukaa na yeye mwenyewe, akafikiri na kutafakari kwa kina bila ya usumbufu.

Siku hizi watu hawataki kujisumbua kabisa, hawataki kupata hata upweke kidogo. Muda wowote ambao wangeweza kuupata kwa ajili yao, unaishia kwenye usumbufu wa simu na mawasiliano.

SOMA; UKURASA WA 308; Kama Ungekuwa Unaishi Jangwani….

Tunakuwa tumeunganishwa na kujiunganisha na wengine kwa kiasi cha kupitiliza, kiasi cha kuleta utengano kwetu binafsi.

Hivyo rafiki yangu, kuwa macho na hili, kuwa makini usiishie kuwa umeungana na wengine lakini umetengana na wewe mwenyewe. Wewe mwenyewe ndiye mtu muhimu sana kwako. Wewe ndiye mshauri mkuu kwako mwenyewe.

Kadiri unavyopata muda wa kuungana na wewe mwenyewe, ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupata njia za kutatua matatizo yako au kuziona fursa za kusonga mbele zaidi.

Tenga muda maalumu kwenye kila siku yako, muda ambao utakuwa na wewe mwenyewe, bila ya usumbufu, mbali kabisa na simu au mitandao. Tafakari maisha yako, kaa na wewe na usijitoroke kwa njia yoyote ile.

Ungana na wewe binafsi kama unavyoungana na wengine.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog