Kuna vitu ambavyo ukivifanya kwenye maisha yako iwe kwa kukusudia au kwa bahati mbaya, lakini kwa sababu unavifanya tu, jiandae kushindwa.

Pengine hujanisikia vizuri,  nimesema kama vitu hivyo unavifanya jiandae kushindwa au kupishana na kila aina inayoitwa fursa ya mafanikio kwa upande wako.

Naomba unielewe, nimesema vipo vitu ambavyo ukivifanya utashindwa tu na mojawapo  vitu hivyo ni kulalamika.

Ikiwa utakaa chini na kutafuta muda wa kulalamika juu ya maisha uwe na uhakika, utalalamika tu, hakuna atakayeweza kukuzuia kuweza kufanya hivyo.

vitabu softcopyNajua utalalamikia kwamba sasa hivi mambo yamekuwa magumu, kila kitu kimebanwa kwako na huoni fursa kama zamani ulivyokuwa ukiziona.

Najua utalalamikia pia mambo mengi sana ambayo ukipewa nafasi ya kuongea, unaweza kuongea hata kwa muda saa mbili na ukaendelea kulalamika moja kwa moja.

Hali hizo unazolalamikia sana ni kweli zipo, lakini malalamiko yako hayo hayawezi kukusadia kufanya kitu chochote zaidi ya kukurudisha nyuma.

Kitu  unachopaswa kufanya badala ya kulalamika unatakiwa kuchukua hatua ya kuweza kubadilisha maisha yako mara moja na si kulalamika tu.

Hakuna mtu ambaye malalamiko ya aina yoyote yale yamemfikisha mbali. Kikubwa hapo utazidi kukakaukiwa na koo lako bure kwa kutumia nguvu nyingi za kulalalimika.

Kutoa malalamiko na visingizo ni vitu ambavyo ukiviendekeza haviwezi kuisha kwenye maisha yako hata kila siku ukitaka kulalamika utalalamika sana.

Itafika mahali utalalamikia serikali inakuonea, utalalamika vitu gharama zake zimepanda, utalalamika bosi wako hakutendei haki na mengine mengi tu.

Ndio maana unaambiwa watu maskini wanafanya sana mambo matatu, jambo la tatu ni kulalamika, la pili ni visingizio na la kwanza jukumu la maisha yao kuwapa wengine.

Malalamiko ukumbuke sio hatua ya kuchukua hata siku moja, chukua hatua halisi, na usifanye malalamiko yako kama ni hatua ya kuchukua kwenye maisha yako.

Ni kweli maisha yanaweza yasiwe na usawa kwako, lakini kwa nini ulalamike badala ya kuchukua hatua juu ya maisha yako ya kila siku?

Unachopaswa kujua ukikazana sana kuendelea kutafuta malalamiko, basi elewa utapishana na fursa nyingi sana kwako yaani hakuna ambacho utaweza kukifanikisha.

Unatakiwa sana kuchukua hatua na kuacha malalamiko kwenye maisha yako, hutafika mbali na hutaweza kuambulia kitu kama utakuwa unaendelea kulalamika tu.

Kitu cha kuelewa ukiendelea kulalamika, utapishana na fursa nyingi za kufanikiwa kwako kwenye maisha yako ya kila siku maana utalalamika na hatua hutachukua.

Kama unafikiri natania, waangalie walalamikaji wazuri kwenye maisha ni watu ambao hawafanikiwi, wanakula matunda ya kulalamika kwao.

Jiulize, unataka kuwa miongoni mwa watu ambao wanalalamika? kama utakuwa ni miongoni mwao itakuwa ngumu sana kwao kuweza kufanikiwa.

Jifunze kuwa mtu wa kuchukua hatua, acha kulalamika kwa jambo lolote hata kama unaona unaonewa.

Matokeo yake angalia ni kipi ambacho unaweza ukafanya ili kikusaidie kuweza kufanikiwa na sio tu kuwa mtu kulalamika bila mpango.

Naamini kwa kufanyia kazi kilichomo katika makala haya utakuwa ni mtu wa hatua na malalamiko kwako itakuwa kama ni kituo cha polisi.

Chukua hatua sahihi, kinyume cha hapo kama unaendelea kulalamika utambue utapishana na fursa kubwa sana za kukusaidia kuweza kufanikiwa kwako.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

http; www.amkamtanzania.com,

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com.