Not how long, but how well you have lived is the main thing. – Lucius Annaeus Seneca
Mwanamafanikio, leo ni siku mpya na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Mwaka huu 2018 tunaongozwa na TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tutaweza kupiga hatua kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Asubuhi ya leo tutafakari; SIYO UREFU WA MAISHA, BALI UBORA WAKE…
Kila mtu anapenda kuwa na maisha marefu, kuishi miaka mingi iwezekanavyo.
Lakini ni wachache sana wanaochukua hatua kuyafanya maisha yao kuwa bora sana.
Ambacho ni muhimu sana kwa kila mtu siyo miaka mingi kiasi gani ameishi, bali maisha aliyoishi yamekuwa na maana kiasi gani kwake na kwa wengine pia.
Kuishi kuda mredu huku ukifanya yale uliyozoea kufanya ni kuishi kwa mateso.
Wapo watu ambao wanaishi mwaka mmoja mara sabini na kusema wameishi miaka sabini. Wakati wanachofanya ni kile kile kila mwaka, ila kwa kurudia rudia kila mwaka.
Ili maisha yawe bora kwako, lazima uwe tayari kufanya vitu vya tofauti, vitu ambavyo wengine hawapo tayari kufanya.
Lazima uchukue hatua za kuwa bora zaidi kila siku, ujaribu mambo mapya ambayo yanaweza kushindwa na uwe na ubunifu wa kipekee.
Mwisho wa siku, hakuna atakayetoka kwenye haya maisha akiwa hai. Hivyo badala ya kukazana kufika kwenye kifo salama, ni vyema kuyaishi maisha halisi kwako. Fanya yale ambayo ni muhimu na ya kipekee, ishinde hofu ya kushindwa na maisha yako yatakuwa bora sana.
Ni vizuri kuishi maisha marefu, lakini kama maisha hayo yatakuwa siyo bora, kama maisha hayo yatakuwa ya kulalamika, kamw maisha hayo yatakuwa ya kufanya mambo kwa mazoea, basi yatakuwa ni mateso makubwa.
Kazana kuwa na maisha bora sana kwako na kwa wengine pia.
Uwe na siki bora sana leo, siku ya kipekee, siku ya kufanya makubwa.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha
Asante kocha kwa tafakari nzuri ya leo, Mungu ni mwema ,tukiacha maisha ya mazoea kuacha alama inawezekana, nakutakia nawe kocha wetu ck njema.
LikeLike
Karibu sana
LikeLike