Kwenye harakati za kutafuta maisha ya mafanikio yapo mambo mengi sana hasi unayokutana nayo na utaendelea kukutana nayo, lakini wito wangu mkubwa kwako ni kwamba hata siku moja usiruhusu mambo hayo yakaweza kukutawala wewe.

Katika maisha yako, upo wakati ambao itatokea utakatishwa tamaa na wengine, lakini hiyo haitoshi hata itafika wakati utajikatisha tamaa mwenyewe kwa kuona huwezi tena kufanikiwa, pia hapa hutakiwi kurusu hali hiyo ikutawale.

Pia kuna wakati utajiona wewe huwezi kufanya kitu na utakuja na visingizio vya kila aina kwamba umeshindwa kufanya jambo hilo kwa sababu hii na ile. Yote hayo yanapotokea simamia imara maamuzi yako na usiyumbe.

Yapo maamuzi ambayo unaweza ukawa nayo wewe inapotokea changamoto. Maamuzi hayo inaweza ikawa ni kweli umeamua sasa kusimama hapo kwa sababu umezuiliwa na changamoto hizo au ukamua kuendelea mbele.

Maisha Hayajawahi

Pia kuna wakati unaweza ukarusu maamuzi yakupatwa na hasira nyingi sana kwa sababu umeuziwa na watu na kusahau kufanya kila kitu kwa siku nzima, au ukazifukia hasira hizo na wewe ukaendelea na mambo yako mengine kwenye maisha, uamuzi ni wako.

Kuruhusu maamuzi ya msingi ndiyo yale yanayoweza yakabadilisha maisha na sio maamuzi ya hivyo, hilo ndilo jambo la msingi kwako. Najua unaelewa ninaposema maaumuzi ya hovyo ni maaumuzi ambayo hayawezi wewe kukusaidia kitu.

Hutakiwi hata siku moja kuendele kuruhusu maamuzi ya hivyo kama ya kuendelea kushikilia woga kwenye maisha yako. Unatakiwa uwe na maamuzi ya kuufutilia mbali huo woga na kutengeneza maisha unayoyataka.

Kati ya kitu ambacho kina uwezo wa kuharibu maisha yako ikiwa utakiruhusu ni maamuzi yako ya hovyo. Kila wakati unatakiwa uwe na maamuzi sahihi na si maamuzi ya hovyo ambayo yanaweza kukuangusha.

Kama nilivyosema unaweza ukaruhusu mambo mengi ikiwa pamoja na hata kuzika ndoto zako  na kusema sana kwamba ndoto zako hawiwezekani kabisa, au ukaamua kuzifanya ndoto zako zikaendelea kuwa hai wakati wote, uamuzi huo unao wewe.

Inapofika mahali ukaamua kuruhusu hali yoyote hasi au hali yoyote ile inayoweza kubomoa maisha yako, basi hapo naweza kusema upo kwenye wakati mgumu au wakati mbaya wa kuweza kurudi nyuma kimafanikio.

Najua unakutana na kukatishwa tamaa, unakutana pia na changamoto nyingi ambazo ukiangalia kiuhalisia ni kubwa kwako, lakini kwako usiruhusu na kufanya maamuzi ya kufanya changaomoto hizo zikawa chanzo cha kushindwa kwako.

Upo hapo kwa ajili ya kushinda si kwa ajili ya kushindwa. Jiwekee maamuzi kwa vyovyote vile itakavyokuwa iwe changamoto kidogo au changomoto kubwa, lakini amua kabisa kutoka moyoni kwako kwamba lazima uwe mshindi.

Ndio, nimesema lazima uwe mshindi pasipo kujali ni kitu gani ambacho umekukuna nacho kwenye maisha yko . Hauruhusiwi hata kidogo kufanya kitu chochote kinachopelekea maisha yako yakawa ya hovyo.

Kumbuka kila siku kuwa makini, kutokurusu maamuzi ya aina yoyote ile kuweza kukurudisha nyuma, iwe changamoto, woga, kukatishwa tamaa au chochote kile. Ukiweza kushinda hali hiyo, jiandae na mafanikio makubwa mbele yako.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com