No man is free who is not master of himself – Epictetus
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri kwetu.
Ni siku mpya ya juma jipya ambapo tumepata nafasi ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ndiyo msingi wetu mkuu wa mafanikio.
TATUA, AMUA NA ONGOZA ndiyo mwongozo wa mafanikio ya maisha yetu kwa mwaka huu 2018.
Asubuhi ya leo tutafakari HAUPO HURU…
Kila mtu anapenda kuwa huru,
Kila mtu anapenda kufanya kile anachotaka kufanya,
Kila mtu anapenda kupanga mambo yake na kupata kile anachotaka.
Lakini haya pekee hayamaanishi uhuru.
Kama mtu huwezi kujidhibiti wewe mwenyewe, kama huwezi kujisimamia wewe mwenyewe, basi haupo huru.
Kama huwezi kupanga kitu na ukajisimamia kukifanya kweli, jua haupo huru.
Kama huwezi kujikataza kufanya kitu na ukafuata hilo kweli basi huna uhuru unaofikiri unao.
Uhuru wa kweli unakuja pale mtu unapoweza kujitawala na kujisimamia mwenyewe.
Kwa sababu hakuna utumwa mkubwa kama utumwa wa mwili na akilo yako.
Anza kujitawala wewe mwenyewe na utaweza kutawala chochote.
Na kushindwa kujitawala wewe mwenyewe, utatawaliwa na chochote.
Nenda ukawe huru leo, kwa kujibana ufanye kile ulichopanga kufanya, bila ya kuahirisha.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha