Kuna maeneo ya maisha yetu, ambayo tunajijua hatupo vizuri, lakini sasa si kweli kwamba hatupo vizuri kama tunavyofikiri.
Kadhalika yapo maeneo ya maisha yetu ambayo tunajijua tupo vizuri, lakini na hapo pia hatupo vizuri kama tunavyofikiri.
Kinachotokea ni kwamba huwa tunajiumiza sana kwa yale maeneo ambayo tunafikiri hatupo vizuri wakati siyo sahihi.
Na kwa yale maeneo ambayo tunafikiri tupo vizuri, tumekuwa tunajikadiria kupitiliza.

Tunakazana kuangalia maeneo ambayo siyo sahihi, tukikazana kuboresha madhaifu yetu, kitu ambacho kinazalisha madhaifu zaidi.
Pia kwa kuamini kwamba kuna maeneo tupo vizuri, tumekuwa tunayachukulia kwa mazoea na kinachotokea ni kukosa ule ubora na umakini tunaofikiri tunao.
Suluhisho ni moja, chagua maeneo gani ambayo unataka kuwa bora zaidi, kisha kila siku piga hatua ya kuwa bora zaidi.
Kila siku jua kipo kitu cha kujifunza, ipo hatua ya kwenda, yapo mambo ya kujifunza.
Ondokana kabisa na dhana ya wapi uko vizuri na wapi uko vibaya, na tengeneza dhana ya kujitengeneza kuwa bora kabisa kwenye yale maeneo muhimu kwa maisha yako.
Kila siku kazana kuwa bora, na hili litakusukuma zaidi ya kufikiria upo vizuri wapi na wapi haupo vizuri.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog