Everything that happens happens as it should, and if you observe carefully, you will find this to be so. – Marcus Aurelius
Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Ni kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio ni TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunakwenda kupiga hatua kubwa mwaka huu 2018.
Asubuhi ya leo tutafakari KINATOKEA KAMA KINAVYOPASWA KUTOKEA…
Kila kitu kinachotokea kwenye maisha yako, kinatokea kama kinavyopaswa kutokea.
Hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya kwenye maisha yako.
Wala hakuna kinachotokea tu bila ya sababu yoyote.
Kila kitu kinatokea kama kinavyopaswa kutokea.
Na ukichunguza kwa makini kila kinachotokea, utagundua kinatokea kutufundisha kitu fulani, kutukumbusha kitu fulani au kutusisitizia kitu fulani.
Hivyo chochote kinachotokea kwenye maisha yako, usikilalamikie au kusema kwa nini kinanitokea mimi tu. Badala yake jiulize nini kinakufundisha, kinakukumbusha au kukusisitizia.
Hata kama umefanya uzembe au makosa na yakapelekea kitu fulani kutokea, ambacho siyo kizuri, kimetokea hivyo ili kukufundisha na kukukumbusha kuwa makini na hatua unaochukua.
Kila kinachotokea kwenye maisha yako, kiwe kizuri au kibaya, kinatokea kaka kilivyopaswa kutokea na ni njia ya wewe kujifunza na kuwa bora zaidi.
Jifunze kupitia kila kinachotokea kwenye maisha yako, na hii itakufanya kuwa bora na kutorudia mambo yale yale.
Ukawe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha
Ahsante kocha wangu tuko pamoja.
LikeLike
Karibu sana James
LikeLike