Wahenga walisema kama unataka kupata ya watu, basi ongea na watu.

Hii ni kauli yenye nguvu sana kwenye maisha ya mafanikio, kwa sababu huwezi kufanikiwa wewe mwenyewe. Chochote unachotaka kwenye maisha yako, kinatoka kwa wengine. Na ili uweze kukipata, unahitaji kuongea na watu.

Dunia nzima inazunguka kwenye kitu kimoja, kuongea na watu, kujua kile wanachohitaji, kuwapatia kisha nao wanakulipa kulingana na kile ulichowapatia.

Furaha

Hakuna chochote kinachokamilishwa kwenye haya maisha, ambacho hakihusishi mazungumzo na wengine. Iwe ni mazungumzo ya ana kwa ana, au kwa njia ya simu, lazima watu muongee, mkubaliane kisha mfikie maamuzi fulani.

SOMA; UKURASA WA 965; Kufanya Vitu Kwa Usahihi Na Kufanya Vitu Sahihi…

Hivyo moja ya vitu ambavyo unapaswa kuvizingatia sana kwenye maisha yako, ni kujua namna bora ya kuongea na wengine. Kujua njia bora ya kuwaeleza watu kile unachofanya au unachotoa, na kuweza kuwashawishi kuchukua hatua.

Hivyo kila fursa unayoipata, zungumza na watu, zungumza na watu unaowajua, pia zungumza na watu usiowajua. Anzisha mazungumzo ambayo yatakuwezesha kuwajua watu zaidi, kujua mahitaji yao na jinsi gani unaweza kuwasaidia kwenye mahitaji hayo.

Mazungumzo ni njia nzuri ya kuwajua wengine, kueleza unachofanya na hata kukuza mtandao wako. Unapopata fursa ya mazungumzo na wengine, itumie vizuri.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog