How much more grievous are the consequences of anger than the causes of it. – Marcus Aurelius
Asubuhi njema mwanamafanikio,
Ni siku nzuri, ya kipekee kwetu kwenda kuyaishi maisha yetu ya msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MATOKEO NI MACHUNGU KULIKO SABABU….
Kuna wakati mambo fulani yanaweza kutokea kwenye maisha yetu, ambayo yanatufanya tupate hasira.
Labda ni kitu kimekwenda tofauti na matarajio yetu, au ni watu wamefanya tofauti na tulivyotegemea au walivyoahidi.
Wakati huo wa hasira huwa tunaona tuna kila haki na ni sahihi kwetu kukasirika, kwa sababu hayukutegemea mambo yaende hivyo.
Lakini sasa, matokeo ya hasira, huwa ni machungu sana ukilinganisha na kilichosababish hasira hiyo.
Yaani ukilinganisha matokeo ambayo mtu unayapata kwa hayua ulizochukua kutokana na hasira ulizokuwa nazo, ni mabaya na yenye madhara kwako, kuliko hata ubaya na madhara ya kile kilichosababisha hasira hiyo.
Hivyo mwanamafanikio, kitu cha kwanza kabisa ni kuhakikisha huchukui hatua ukiwa na hasira, maana matokeo yake hutayaweza, na hayatalingana na sabau ya hasira hizo.
Kufanya maamuzi au kuchukua hatua wakati una hasira, ni sawa na kuweka mafuta ya ta kwenye moto ambao ni mdogo, unazidisha moto na madhara yake pia.
Kumbuka hili mara zote unapojikuta kwenye hali ya kukwama, kukwazika na kukasirishwa. Kuchukua hatua wakati kama huo ni kutengeneza matokeo mabovu kuliko hata kile kilichosababisha hasira.
Jipe muda, pumua na kuwa na subira, utaona hatua sahihi za kuchukua hasira ikishatulia.
Uwe na siku bora na ya kipekee sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha