Anything in any way beautiful derives its beauty from itself and asks nothing beyond itself. Praise is no part of it, for nothing is made worse or better by praise. – Marcus Aurelius

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii mpya na ya kipekee kwetu,
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
TATUA, AMUA NA ONGOZA ndiyo mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio mwaka huu 2018 ambapo tunakwenda kufanya makubwa sana.

Aaubuhi ya leo tutafakari SIFA HAIONGEZI UZURI WA KITU…
Wapo watu ambao wanakazana kufanya vitu vizuri sana kwenye maisha yao, lakini hakuna mtu ambaye anawasifia kwa kile wanachofanya.
Hilo linawakatisha tamaa, na kuona labda wanachofanya siyo kizuri.

Sifa haiongezi au kupunguza uzuri wa kitu.
Uzuri wa kitu unatoka ndani ya kitu hicho, na siyo nje ya kitu hicho.
Hicyo kama kitu ni kizuri, ni kizuri hata kama hakuna anayekisifia.
Na kama kitu siyo kizuri, kitaendelea kuwa siyo kizuri hata kama kila mtu anakisifia.

Fanya kilicho kizuri, fanya kilicho sahihi na kamwe usitake watu wasifie ndiyo uamini kitu ni kizuri au sahihi.
Wewe unajua kizuri na sahihi ni kipi, hivyo weka juhudi kwenye kifanya.

Uwe na siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha