Natural ability without education has more often raised a man to glory and virtue than education without natural ability. – Marcus Aurelius

Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio?
Hongera kwa nafasi hii nyingine nzuri ya leo.
Ni siki ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunaweza kufanya makubwa sana kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari ELIMU BILA YA UWEZO WA ASILI…
Kosa moja ambalo limekuwa linafanyika kwenye elimu ni kuamini mwanafunzi ni mtupu na hivyo anatakiwa kujazwa maarifa na ujuzi mpya.
Kwa kufanya hivi, mfumo wa elimu unasahau kwamba kila mtu ana uwezo wa asili, uwezo mkubwa sana ambao upo ndani yake.

Kwa mtu kujua na kutumia uwezo huo, anaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yake.
Yaani kama mtu atapata elimu, hata iwe kubwa kiasi gani, kama hatajuanna kutumia uwezo mkubwa na wa asili uliopo ndani yake, elimu haitakuwa na msaada kwake.
Lakini kama mtu atajua na kuweza kuutumia uwezo mkubwa na wa asili uliopo ndani yake, hata kama hatapata elimu, anaweza kufanya makubwa sana.

Sasa jiulize vipi kama mtu atapata elimu kubwa, halafu ajue na kuweza kutumia uwezo mkubwa na wa asili uliopo ndani yake, mtu wa aina hii hataweza kushikika.

Jukumu lako kubwa na la kwanza kabisa ni kujua na kuweza kutumia ule uwezo mkubwa na wa asili uliopo ndani yako.
Vile vitu watu wanaita vipaji, vile vitu ambavyo unavipenda na kuvifuatilia sana, vile vitu ambavyo upo tayari kufanya hata kama hakuna anayekulipa.
Angalia jinsi gani unaweza kuvifanya kwa njia ambayo utaongeza thamani kwa wengine na kuweza kutengeneza kipato pia.

Ukiweza kutumia uwezo wa asili uliopo ndani yako, halafu ukachanganya na elimu uliyonayo au unayoendelea kupata, utapiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.

Uwe na siku bora sana leo, siku ya kutumia uwezo mkubwa na wa asili uliopo ndani yako.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha