Watu huwa wanalalamika kuumizwa na watu au vitu wanavyopitia kwenye maisha yao.

Lakini katika kila hali ambayo watu wanalalamikia inawaumiza, wapo wengine ambao wanaendelea na maisha yao vizuri bila ya kulalamika kuumizwa.

Iwe ni kwenye mahusiano, kazi na hata biashara, kuumizwa ni kuchagua. Pale unapochagua kuangalia kile kinachokutokea kama ni kibaya, basi utaumia. Lakini ukichagua kuangalia kila kinachotokea kama sehemu ya maisha, unajifunza na kupiga hatua zaidi.

Kujilinganisha

Mateso kwenye maisha ni kitu cha kawaida, kuna wakati utakosa unachostahili kupata, kuna wakati utaweka juhudi na wengine wakanufaika kupitia juhudi zako na wewe usipate chochote. Kuna wakati wengine watafanya makosa na lawama ukapewa wewe.

SOMA; UKURASA WA 577; Vipo Ndani Ya Uwezo Wetu….

Yote hayo ni mambo mabaya, lakini kuumia ni chaguo lako mwenyewe. Kama ukichagua kuangalia kila tukio kama sehemu ya maisha na njia ya kujifunza, utajifunza na kuwa bora zaidi.

Lakini kama utachukua kila hali kama maumivu kwako, kila wakati utaumia na kujiona usiyestahili.

Chagua kutokuumia na hakuna yeyote au chochote kitakachoweza kukuumiza.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog