“I should say that happiness is being where one is and not wanting to be anywhere else.” — Michael Frayn
Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipeke kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
TATUA, AMUA NA ONGOZA ndiyo mwongozo wetu wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2018.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA UNAFIKIRIA KUWA SEHEMU NYINGINE, HAUPO SEHEMU SAHIHI…
Ipo njia rahisi sana ya kujua kama kitu tunachofanya ni muhimu na sahihi kwetu.
Na njia hiyo ni kuangalia kipi tunachofikiri kwa wakati huo.
Kwa mfano kama wakati unafanya kazi yako, mawazo yako yapo kwenye kitu kingine tofauti, basi kazi unayoifanya siyo muhimu kwako.
Kama wakati unapumzika unafikiria ungekuwa unafanya kazi, basi mapumziko unayofanya siyo muhimu kwako.
Kama biashara unayoifanya, muda mwingi unafikiria biashara nyingine basi hiyo siyo muhimu kwako.
Kitu kinapokuwa muhimu kwako, kinabeba mawazo na fikra zako zote. Huwezi kufikiria kitu kingine kwa wakati ambao unafanya kile ambacho ni muhimu zaidi kwako.
Hivyo jifunze kuweka mawazo yako yote kwenye kile unachofanya, maana hivyo ndivyo unavyojengw umuhimu wa kitu.
Na kama huwezi kuweka mawazo yako kwenye kile unachofanya, chagua kufanya kingine, maana haitakuwa na msaada kwako.
Uwe na siku njema leo, mawazo yako yote yawe kwenye chochote unachofanya.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha