“Difficulties are things that show a person what they are” – Epictetus

Hongera rafiki kwa siku hii nzuri na ya kipekee kwetu,
Ni siku mpya ambapo tumepata nafasi mpya ya kwenda kuweka juhudi kubwa kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UTAWAJUA WATU KWENYE UGUMU…
Wakati mambo yanakwenda vizuri, kila mtu anaweza kuigiza anachotaka.
Kila mtu anaweza kuahidi na kutimiza chochote pale mambo yanapokuwa rahisi.

Ni wakati wa ugumu ndiyo utazijua tabia halisi za watu.
Ni wakati wa changamoto na matatizo ndiyo utaziona sura halisi za watu.
Kwa sababu wakati huo ni vigumu kuigiza, na siyo rahisi kutekeleza kile ambacho mtu ameahidi.

Hivyo nyakati ambazo mambo ni magumu, ndiyo nyakati unazopaswa kuwajua watu vizuri.
Pia ndiyo nyakati za kujijua wewe vizuri.
Kwa sababu kama hujawahi kukutana na ugumu, huenda hata wewe mwenyewe hujijui vizuri, hujui ni kwa kiasi gani unaweza kujisukuma na hujui ni uvumilivu kiasi gani unaweza kuweka.

Waelewe watu kwenye nyakati rahisi,
Wasikilize watu kwenye nyakati rahisi,
Lakini kuwajua kweli watu, ni kwenye nyakati ngumu, nyakati za changamoto, maana nyakati hizo, ni vigumu kuigiza.

Uwe na siku bora sana ya leo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha