Uhalisia ni kifo cha mafanikio, pale unapopanga kitu na kuanza kujiuliza kama kinaendana na uhalisia au la, ndiyo mwisho wako wa kwenda mbali zaidi.
Huwa tunapenda kuweka mipango ya kawaida, mipango inayoendana na kile tulichozoea, mipango inayowezekana na inayoendana na uhalisia.
Mtu mmoja amewahi kusema, watu wa kawaida huwa wanaenda kama dunia inavyotaka waende, lakini watu wasio wa kawaida huwa wanaipeleka dunia vile wanavyotaka wao iende. Na hivyo maendeleo yote yanatokana na watu wasio wa kawaida.

Kama utapanga yale ambayo ni ya kawaida, yaliyozoeleka na yanayowezekana, tuna uhakika wa jambo moja, hutakuja na matokeo mapya na ya tofauti. Huenda usishindwe, lakini pia hutashinda.
Lakini pale unapoweka mipango isiyo ya kawaida, mipango ambayo kwa uhalisia inaonekana haiwezekani, hapo ndipo unapojiweka kwenye hatari kubwa ya kushindwa, lakini pia unajiweka kwenye nafasi ya kufanikiwa zaidi.
SOMA; Maajabu Ya RIBA MKUSANYIKO (COMPOUND INTEREST) Katika Kujijengea Utajiri.
Kitendo cha kupanga makubwa na yasiyowekezana, kinakusukuma kuchukua hatua kubwa ana ambazo hazijazoeleka, hatua hizo tu zinakuwezesha kupata matokeo tofauti na uliyozoea kupata. Hata kama hutapata kile ulichongana, bado matokeo utakayopata yatakuwa makubwa kuliko ambayo umezoea kupata.
Mwisho, kama ulivyo usemi maarufu, kama hakuna anayekushangaa, kama hakuna anayekuambia unachopanga hakiwezekani au utashindwa, basi jua hakuna makubwa unayopanga au kufanya.
Anza sasa kuweka malengo na mipango isiyo ya kawaida, weka malengo na mipango mikubwa zaidi ya ulivyozoea, na anza kuchukua hatua. Mfano, kwenye kipato, anza na mpango wa kupata mara kumi ya kipato unachopata sasa, halafu anza kuchukua hatua kubwa zitakazokuwezesha kupata mara kumi. Hata kama hutapata mara kumi, utapata mara 5 au hata mara 2, ambayo ni bora kuliko sasa.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog