Ni asili ya binadamu kupenda raha, kupenda kile kinacholeta manufaa ya haraka kuliko kile ambacho manufaa yake yanachelewa.
Lakini sheria ya asili ni hii, chochote kinachokupa raha leo, kesho kitakupa maumivu. Ni sheria ya asili, ambayo huwezi kubishana nayo na wala huwezi kuikwepa.

Jaribu kuangalia mifano kwenye kila eneo la maisha, utaona jinsi ambavyo watu wengi wanatengeneza matatizo ya maisha yao kwa kuendekeza raha za muda mfupi na ambazo wala hazidumu.
Mtu anakunywa pombe leo, akipata raha ya muda mfupi, kwa ulevi anaopata, lakini maumivu yake atayapata siku zijazo, pale ulevi unapokuwa tabia ambayo hawezi kuachana nayo tena, pale ulevi unapomletea magonjwa na hata unapompotezea fedha.
RAHA; UKURASA WA 1108; Maumivu Ni Sehemu Ya Mchezo…
Mtu anapata raha ya mshahara kwenye ajira leo, lakini kesho unakuwa maumivu, pale anapokuwa tegemezi kwenye mshahara huo, halafu unakuwa hautoshelezi na hawezi kuachana na mshahara huo.
Hivyo tunapaswa kuwa makini sana na kila hatua tunayochukua leo, tuhakikishe tunaelewa matokeo yake kwa kesho na siku zijazo.
Usikimbilie kufanya mambo leo kwa sababu yanakupa raha au ndiyo rahisi kufanya, halafu yakaja kuwa maumivu kwako kesho.
Haimaanishi kwamba hatupaswi kufanya vinavyotupa raha, ila kabla hatujafanya, tujiulize kile tunachofanya leo kinatengeneza nini kesho?
Lengo kuu la maisha ni furaha, ambayo inatokana na kuyaishi maisha kwa ukamilifu wake. Tunapoanza kung’ang’ana na raha, ndiyo tunavuruga kila mpango wa furaha tulionao.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog