Rafiki,

Karibu kwenye utaratibu wetu wa kujisomea vitabu ambapo kila mwezi nimekuwa nakushirikisha kitabu kizuri kwako kujisomea ili kuweza kujifunza na kupiga hatua kwenye maisha yako.

Kila mwezi nimekuwa nakushirikisha kitabu cha kusoma, ambacho maarifa yake yanakupa mbuni ha hamasa ya kufanikiwa zaidi kwenye chochote unachofanya.

Pia nimekuwa nakupa njia bora ya kuweza kuhakikisha unamaliza kusoma kitabu kimoja kila mwezi, kwa kukukaribisha kwenye kundi la KURASA KUMI, ambapo kila siku unasoma kurasa kumi na hivyo ndani ya mwezi mmoja unakuwa umemaliza kitabu.

Mwezi Mei  2018 nakushirikisha usome kitabu cha siri 177 za watu wenye mafanikio makubwa zaidi. Hichi ni kitabu ambacho kimefanyiwa utafiti kwa kuwaangalia wale ambao wanafanikiwa zaidi, wanaofanikiwa kawaida na wanaoshindwa, ili kujua nini kinatofautisha makundi hayo.

177-mental-toughness-secrets-of-the-world-class

Mwandishi wa kitabu 177 MENTAL TOUGHNESS SECRETS OF THE WORLD CLASS, Steve Siebold, kupitia utafiti na kushirikiana kwake na watu waliofanikiwa zaidi, amefanikiwa kutushirikisha siri hizo 177.

Uzuri wa siri hizi 177 ni kwamba siyo siri kihivyo, ni vitu vya kawaida sana ila vinachukuliwa kwa nidhamu ya hali ya juu. Pia kwenye siri hizo 177 hakuna inayokutaka uwe na elimu  kubwa, uwe umetoka familia tajiri au hata uwe na fedha.

Popote pale ulipo, unaweza kuanzia hapo na ukafanikiwa sana kama utazijua siri hizi 177 na kuziishi kwa uhalisia kwenye maisha yako.

MAKUNDI MATANO YA WATU KIFIKRA NA KIMAFANIKIO.

Kwenye kitabu hichi, Steve anawagawa watu kwenye makundi au ngazi tano kulingana na fikra zao na mafanikio pia. Makundi hayo ni kama ifuatavyo;

Moja; Kundi la masikini; hawa ni wale ambao hawajui watakula nini kesho, maisha yao ni magumu na hawana kipato cha uhakika.

Mbili; Kundi la wafanyakazi; hili ni kundi la wale ambao wana kazi, lakini kipato chao hakitoshelezi mahitaji yao. Hivyo maisha yao yanakuwa magumu na wanakuwa wamekwama kwenye kazi wanazofanya, wasione namna ya kupiga hatua zaidi.

Tatu; kundi la kati, hili ni kundi ambalo ni la wafanyakazi, ila kipato chao ni kikubwa na kinawawezesha kuwa na maisha bora, kwa kukidhi yale mahitaji muhimu. Ila pia kundi hili bado linakuwa na changamoto kwa sababu mahitaji yao yanakua kwa kasi na hivyo kujikuta kwenye madeni mengi na hivyo wanakuwa watumwa wa kazi, hawawezi kuziacha kazi zao maana ndiyo wanategemea kuendesha maisha yao.

Nne; kundi la juu, hili ni kundi ambalo lina fedha nyingi kuliko mahitaji waliyonayo, ni kundi ambalo linakuwa na akiba ya kutosha, lakini bado wanakuwa hawajaridhika na mafanikio wanayokuwa wameyapata. Bado ndani yao wanajiona hawajafika wanakotaka kufika, na mara nyingi wapo kwenye hali ya mashindano.

Tano; kundi la mafanikio ya juu zaidi, hili ni kundi la juu zaidi, kundi ambalo maisha yao yamefikia mafanikio ya juu kabisa na wameridhika na mafanikio hayo. Kundi hili lina mafanikio kwenye kila eneo la maisha, kifedha, kiafya, kimahusiano na kiimani. Ni kundi ambalo halishindani, wala kuishi maigizo, bali kundi linaloishi uhalisia wa maisha.

Katika kitabu chote, mwandishi analinganisha makundi mawili, kundi la kati, ambapo kama unasoma hapa kwa nafasi kubwa upo kwenye kundi hilo, na kundi la mafanikio ya juu zaidi.

Lengo la mwandishi ni uweze kutoka kwenye kundi la tatu, ambalo ni gereza kwa wengi na kufika kundi la juu zaidi ili uweze kuwa na maisha ya uhuru wa hali ya juu.

Kwa kuzijua siri hisi 177 na kuziishi, utaondoka kwenye kundi lolote ulilopo sasa na kufika kwenye kundi la juu zaidi. Na ninachokuambia ni hichi, siri hizi 177 siyo nyingi na wala siyo ngumu, unachohitaji ni nidhamu tu kuziishi.

Mwandishi pia ametoa tofauti 25 za watu wa kundi la kati, au kama tunavyoweza kusema watu wa kawaida na wale ambao wamefanikiwa zaidi. Kama hutasoma kitabu kizima, basi nakuomba sana rafiki yangu, soma ukurasa wa 23 na 24 kisha tafakari tofauti hizo 25 na kwa hakika utaona jinsi ambavyo wewe mwenyewe umekuwa unajizuia kufanikiwa.

Nilisoma kitabu hichi kwa mara ya kwanza miaka 5 iliyopita, lakini nimekuwa nakirudia mara kwa mara, na hata nikikosa muda kabisa, basi narudia ukurasa wa 23 na 24, kwa kuzisoma tofauti 25 za waliofanikiwa zaidi na wale wa kawaida, ili kuhakikisha najikumbusha na kutokurudi nyuma. Kwa sababu ni rahisi sana kurudi nyuma kama huchukui muda wa kujikumbusha yale muhimu.

Wito wangu kwako rafiki yangu, mwezi huu wa mei, soma kitabu hichi na ishi kila siri unayoisoma. Unaweza kusoma siri sita kila siku moja na kutafakari jinsi unavyoweza kuziishi, na ndani ya mwezi utakuwa umemaliza siri zote 177. Siri hizi ni fupi sana na siyo vitu vipya, hivyo utakachohitaji ni nidhamu ya kuziishi.

KARIBU KWENYE PROGRAMU YA KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU.

Kama unajiuliza utapata wapi kitabu hichi na utawezaje kukisoma wakati wewe huna muda kabisa, nipo hapa kukuambia kwamba, unao muda wa kutosha kusoma kitabu hicho, ni vile tu hujaweza kuupangilia vizuri.

Ninayo program maalumu kwako ya KUSOMA KURASA 10 kila siku, na hivyo kwa mwezi unakuwa umesoma kurasa 300 ambazo ni sawa na kitabu kimoja.

Kwa programu hii, unaingia kwenye kundi maalumu la wasap ambapo unakutana na wasomaji wengine na kujifunza kupitia wao pia. Kila siku unasoma kurasa kumi na kushirikisha kwenye kundi yale ambayo umejifunza.

Ili kupata nafasi ya kuingia kwenye kundi hili, unalipa ada ya shilingi elfu 10 ambayo unalipa mara moja pekee. Ukilipa ada hii unaingia kwenye kundi hili na utapata vitabu vingi vizuri vya kujisomea, pamoja na kujifunza kupitia usomaji wa wengine.

Kujiunga na Programu hii, tuma ada, tsh 10,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 majina yatakayokuja ni AMANI MAKIRITA. Ukishalipa ada, tuma majina yako kamili na ujumbe KURASA KUMI kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253.

Karibu sana tusome kwa pamoja, karibu sana tujifunze siri za kufikia mafanikio makubwa.

Nikusihi tena rafiki yangu, hakikisha unasoma kitabu hichi, na hata kama ulishakisoma huko nyuma, rudia tena kukisoma. Na kama huna muda kabisa wa kusoma, basi rudia kusoma ukurasa wa 23 na 24 ambazo zimeeleza tofauti 25 baina ya wanaofanikiwa zaidi na wale wanaoishia kuwa kawaida.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Usomaji