“Dream no small dreams for they have no power to move the hearts of men.” -Johann Wolfgang von Goethe
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NDOTO KUBWA…
Rafiki, unatakiwa ulipe shilingi ngapi ili uruhusiwe kuwa na ndoto kubwa?
Au unatakiwa upewe ruhusa na nani ndiyo uthubutu kuwa na ndoto kubwa?
Kwa sababu watu wengi wanaogopa sana kuwa na ndoto kubwa kama vile kuna ruhusa hawajapewa na watu fulani.
Iko hivi rafiki,
Akili inayofikiria ndoto ndogo ndiyo hiyo hiyo inayohitajika kufiiria ndoto kubwa.
Na nguvu unazoweka kufanyia kazi ndoto ndogo ndizo utakazohitaji kuwka kufanyia kazi ndoto kubwa.
Ila sasa, ndoto ndogo ni mzigo kwao, kwa sababu haikusukumi sana kama ndoto kubwa inavyoweza kukusukuma.
Kwa kuwa huhitaji kulipia gharama yoyote kuwa na ndoto kubwa,
Pia kwa kuwa huhitaji ruhusa ya yeyote ndiyo uweze kuwa na ndoto kubwa,
Basi usikubali kabisa kuwa na ndoto ndogo.
Muda wowote ota ndoto kubwa, fikiria mipango mikubwa.
Na sehemu nzuri ya kuanzia, ni mara kumi ya ulipo sasa.
Kile unachofikiria sasa, ile ndoto uliyonayo sasa, mipango unayofanyia kazi sasa, ZIDISHA MARA KUMI.
Zidisha mara kumi halafu anza kwa kuchukua hatua sahihi za kufikia hiyo mara kumi.
Ukawe na siku bora rafiki, usisahau;
#ZIDISHAMARAKUMI
#SKININTHEGAME
#WHATEVERITTAKES
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha