Kinapaswa kuwa wewe, kinapaswa kujifanya kuwa bora kila siku unayoanza kuliko ulivyokuwa siku iliyopita. Kinapaswa kujifunza vitu vipya. Kinapaswa kuwa mbunifu zaidi kuliko siku zilizopita.
Cha kwanza unachofikiria kufanya pale unapoamka, pale unapopata muda wa bure ambao huna cha kufanya, hicho ndiyo umekipa kipaumbele kwenye maisha yako.

Sasa hebu chukua muda na fikiria kwa makini, kipi cha kwanza unafanya kila unapoamka? Pale unapowahi mahali na kupata muda mfupi wa kusubiri, unautumia kufanya nini?
Kwa wengi wanaianza siku kwa kufungua simu zao, kuzurura kwenye mitandao ya kijamii, kufuatilia habari. Mtu amekaa kwenye foleni na cha kwanza anachofanya ni kutoa simu yake kuangalia nini kinaendelea, na siyo kuangalia jinsi gani anaweza kuwa bora zaidi.
SOMA; UKURASA WA 942; Kinachokupoteza Ni Vipaumbele…
Unahitaji kujua vipaumbele vya maisha yako na kuvisimamia kwa ukaribu, kuvipa kipaumbele hasa. Unapoianza siku unaianza kwa vipaumbele vyako, na kila unapopata nafasi ambayo huna cha kufanya, fanya kile kipaumbele chako.
Ukipata hata dakika 15 tu, zitumie vizuri, zitumie kujifunza, zitumie kufikiri njia bora ya kufanya kitu.
Jua vipaumbele vyako na vifanyie kazi kwa usahihi, maana vipaumbele hivyo ndiyo vinakutofautisha na wengine na kukufanya wewe kuwa bora zaidi.
Hakuna mtu anakuwa bora kwa kuzurura kwenye mitandao ya kijamii au kujua kila habari inayotokea, yote hayo ni ya kupita na hayana matokeo makubwa kwa yeyote.
Hivyo zingatia sana vipaumbele vyako na sema hapana kwa mengine ambayo hayana mchango kwenye vipaumbele vyako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog