Watu wengi walio na furaha katika maisha yao ni wale waliochagua kuwa na furaha. Furaha ni kuchagua na ni tabia pia. Tabia ambayo tunapenda kuzianzisha katika maisha yetu basi tunatumia siku ishirini na moja tu kuwa na tabia mpya kadiri ya wataalamu. Rafiki, huoni ni kitu kizuri hicho siku 21 tu tabia ambayo inakufanya uwe na maisha ya ajabu unakwenda kuizika kabisa ndani ya siku ishirini na moja.

Wengine hatujui kutoafutisha kati ya furaha na raha sasa wengi tunapopata raha tunajihisi tuna furaha. Mara nyingi furaha huwa ni kitu cha kudumu lakini raha ni kitu cha muda mfupi sana.

Karibu sana rafiki, nikushirikishe sababu tatu zinazowafanya watu wengi kukosa furaha katika maisha yao.

Furaha

Afya duni, afya nzuri haikupi wewe furaha lakini afya duni au mbovu ni sababu ya wewe kutokuwa na furaha. Iwe ni afya yako au ya mwingine ikiwa duni huwa inachangia kutokuwa na furaha.

SOMA; Sababu Kumi (10) Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Furaha Sasa Hivi, Bila Ya Kujali Upo Wapi Au Una Nini.

Sababu ya pili ni kujilinganisha na wengine. Kujilindanisha na wengine ni hasara kubwa sana kwanza inakatisha watu tamaa licha ya kuchangia watu pia kutokuwa na furaha. Tunapojilinganisha na wengine huwa inaathiri furaha zetu.

Tunapojilinganisha na wengine tutaanza kuangalia sisi tukoje na tuna nini nah ii hali ya ulinganisho ndiyo inapelekea hisia za kutokua na furaha.

Katika zama hizi za taarifa, mitandao ya kijamii imekuwa inachangia watu sana kujilinganisha na wengine. watu wanavyoposti picha zao, wakiwa katika sehemu nzuri na mtu akijiangalia na na maisha yake basi huwa anajiona yeye hana maisha wengine ndiyo wana maisha. Kumbe , mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu ya kuuza mazuri tu siyo mabaya, hakuna mtu anayeweza kuweka habari zake mbaya, hata kupiga picha kuonesha mazingira yake halisi. Wengine maeneo wanayoyaweka yanakuwa si halisi kwao hivyo ni mtindo wa kuigiziana tu lakini watu ndiyo wanaumizana hapo na kukosa furaha zao.

Sababu ya tatu ni kuwa na zaidi na kumiliki zaidi. Tunajidanganya kuwa tunapokuwa na zaidi au tunapomiliki vitu vingi zaidi ndivyo tunavyokuwa na furaha lakini ukweli ni kwamba kuwa na zaidi na kumiliki zaidi siyo kwamba inaongeza furaha zetu.

Kuwa na zaidi na kumiliki zaidi huwa haituongezei furaha lakini inatusababishia au kututengenezea sisi mazingira ya kutaka zaidi. Kwa mfano, utamsikia mtu nikiwa na kitu fulani nitakuwa na furaha, nikiwa na fulani nitakuwa na furaha hivyo tumekuwa ni watu wa kusogeza furaha zetu mbele kila siku.

SOMA; Njia Kumi (10) Za Kuyafanya Maisha Yako Kuwa Rahisi Bila Ya Kuyarahisisha.

Ukiweka furaha yako kwenye vitu ukiamini kuwa ukiwa na zaidi ndiyo utakua na furaha unajidanganya badala yake unaongeza tu hali ya tamaa ya kuwa na kumiliki aina ya kitu fulani zaidi.

Tunatakiwa tusifungwe na sababu hizi katika maisha yetu, tuondoke katika vifungo vya kujitakia na tuwe huru sasa. Maisha ni furaha, furahia hapo ulipo na kile ambacho unacho sasa ifikie mahali uache kujilinganisha na mwingine na uishi na kufurahia maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo,epuka sababu ya furaha yako isibebwe na vitu vya nje bali sababu ya furaha yako itoke ndani yako, mazingira yoyote yasiwe ni sababu ya kutokuwa na furaha  kwenye maisha yako.

Kwahiyo, muepuke mwizi mkubwa wa furaha yako ambaye ni kujilinganisha. Kujilinganisha na wengine amekuwa ni mwizi wa furaha za watu wengi katika zama hizi za taarifa zilizo jaa kila aina ya kelele.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !