“The way is long if one follows precepts, but short… if one follows patterns” – Lucius Annaeus Seneca

Siku mpya,
Siku njema,
Siku ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na TATUA, AMUA NA ONGOZA ndiyo msingi tunaouishi leo na kila siku ya maisha yetu, unaotuwezesha kufanya makubwa zaidi.

Asubuhi ya leo tutafakari NJIA NDEFU NA NJIA FUPI..
Njia inakuwa ndefu pale unapofuata maagizo,
Kwa sababu maagizo hayana msimamo, na mara nyingi yanabadilika.
Maagizo yanaweza yasieleweke kutokana na anayetoa maagizo hayo.
Na maagizo mara nyingi yanakuwa kama kitu cha kulazimishwa, hivyo mtu hahamasiki kuchukua hatua, au anafanya kwa shingo upande.

Njia inakuwa fupi pale mtu anapofuata mfumo, anapofuata msingi ambao upo na unaeleweka kuleta matokeo bora.
Kwa kufuata msingi mzuri, mtu anaweza kupata chochote anachotaka, hata kama mambo ni magumu kiasi gani.
Mfumo na msingi unaleta matokeo yanayotarajiwa na hivyo unampa mtu hamasa ya kuchukua hatua zaidi.

Usiendeshe maisha yako kwa maagizo, usijipangie vitu kwa maagizo, badala yake endesha maisha yako kwa mfumo na msingi ambao utakuletea yale matokeo unayotaka kupata. Hii itafanya njia iwe fupi na usipoteze muda kwa mambo yasiyo ya msingi.

Uwe na siku bora sana leo, siku ya kufuata msingi na siyo maagizo.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha