“We will never have more of what we truly desire until we become fully thankful for what we have.” – MICHAEL HYATT

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Ni kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUPATA ZAIDI, SHUKURU KWANZA…
Kila mtu huwa anapenda kupata zaidi kwenye yale mazuri yanayotokea kwenye maisha yake.
Lakini wengi wamekuwa hawapati zaidi, kile kidogo wanachokuwa wamepata kinakuwa kama sumu kwao, inayowazuia wasipate zaidi.

Ili kupata zaid kile mabacho mtu unataka, unahitaji kushukuru kwanza.
Shukuru kwa kile ambacho tayari unacho, hata kama ni kidogo kiasi gani.
Unaposhukuru unaiambia dunia kwamba unajali, unaiambia dunia kwamba kuna utele na hakuna uhaba, unaiambia dunia kwamba upo tayari kupata zaidi na zaidi.

Usiposhukuru unakuwa unaongozwa na hofu, ukifikiri kwamba kuna uhaba na ulichonacho kitapotea muda siyo mrefu. Unajifungua badala ya kukua zaidi, kwa sababu huamini kama unaweza kupata zaidi.

Kuwa mtu wa shukrani mara zote, shukuru kwa chochote ulichonacho, na kuwa tayari kupokea zaid na zaidi.
Dunia ina kila unachotaka, ila inahitaji wewe utake na uwe tayari ndiyo ikupe.
Hatua ya kwanza ya kuwa tayari ni kuwa mtu wa shukrani.

Ukawe na siku bora leo, siku ya kushukuru kwa kuanza na kile ambacho tayari unacho, badala ya kuangalia nini umekosa.

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha